WATUMISHI WA RS MWANZA WAPEWA SOMO SAMIA INFRASTRUCTURE BONDI
Benki ya CRDB imetoa wito kwa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza kuchangamkia fursa za kununua Bondi za Samia ili kutanua wigo wa kipato chao kwa kiwango kikubwa.
Akizungumza na wafanyakazi hao mapema leo asubuhi Januari 10, 2025 kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Meneja mahusiano biashara za Serikali, Bi. Joyce Mruba amebainisha kuwa bado watu wengi hawajafahamu umuhimu na faida za kununua bondi lakini ni utaratibu wa uhakika wa kujiongezea fedha kutegemeana na fedha uliyoweka.
"Wengi tuna kasumba ya kukimbilia kununua magari ya kifahari au nyumba mara tunapopata fedha, hiyo siyo njia sahihi ni sawa na kutupa fedha lakini bandi ni biashara nzuri ya kuzungusha fedha." Amesema.
Ameongeza kuwa unapoweka bondi ya Samia Tshs. Milioni kumi unaweza kupata mkopo wa Tshs. Milioni 8 hivyo kuweza kufanya shughuli zako za kiuchumi kwa uhakika na baada ya muda wa miaka miaka mitano unarudishiwa fedha zako za bondi.
"Benki ya CRDB ni taasisi imara yenye mtaji mkubwa hivyo hakuna sababu ya watu wenye nia ya kuwekeza na benki hiyo kuingia shaka pengine kufilisika hivyo wachangamkie fursa." Ameongeza.
Akitoa neno fupi la shukrani kwa benki hiyo,Katibu Tawala Msaidizi Rasilimali watu na Utawala Bw.Daniel Machunda ameishukuru taasisi hiyo kwa kuzidi kuwa wabunifu hali inayoletwa tija kwa wateja wake na kuzidi kuaminiwa.
"Leo mmetupa somo la Bondi ni dhahiri utaratibu mzuri ambao utawafanya wafanyakazi wasiishi kinyonge na badala yake kuwa na uhakika wa kujiongezea zaidi vipato vyao kwa njia hiyo ya kisasa,"Machunda
Benki ya CRDB imeshinda zabuni ya miaka mitano ya Samia Infrastructure bond mwishoni mwa mwaka jana.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.