WAZALISHAJI WA MAZIWA MWANZA WAPEWA SOMO LA KUBORESHA BIDHAA
Kaimu Katibu Tawala Uchumi na Uzalishaji Bw. Petet Kasele amefungua mafunzo ya elimu kwa wazalishaji wa maziwa Mwanza na kuwataka kuzingatia sheria taratibu ili wawe wazalishaji bora na kulimudu soko la ushindani.
Akifungua mafunzo hayo leo Novemba 7, 2024 kwenye ukumbi wa Nyanza Kasele amebainisha kuwa bado baadhi ya wazalishaji wa maziwa wanapata changamoto na kujikuta wakati mwingine kulipa adhabu ya malipo ya fedha au kufungiwa kutokana na kutofuata miongozo iliyopo.
Amesema Serikali ya Mkoa wa Mwanza kwa kutambua umuhimu wa tasnia ya maziwa imeendelea kuboresha mashamba ya ng'ombe bora wa mitamba pamoja na kuhamasisha kilimo bora cha malisho ya ng'ombe.
"Uzalishaji wa maziwa mkoani Mwanza katika mwaka 2023/2024 ulifikia lita 398.53 na tuna jumla ya mashamba makubwa 15 ya ng'ombe wa maziwa na kuanzishwa viwanda vidogo 13 vya kuchakata maziwa",Kasele.
Kwa upande wake mteknolojia wa chakula kutoka bodi ya maziwa, Israel Mwingira amesema mafunzo hayo yatawasaidia wazalishaji hao hasa wanapotaka kuuuza au kuagiza maziwa nje ya nchi.
"Wazalishaji wengi maziwa wanafanya shughuli zao bila kujisajili na inapobainika wanajikuta wanakumbana na mkondo wa sheria na kuona kama wanaonewa",Nice Nestory,mwanasheria,bodi ya maziwa
Wazalishaji hao wameelimishwa kuhusu sheria ya tasnia ya maziwa,taratibu za usajili na taratibu za kuomba vibali vya kutoa au kuingiza maziwa nchini.
"
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.