WAZIRI KIKWETE ASHIRIKI MBIO ZA HISANI YA KUMBUKIZI YA MWL NYERERE
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Mhe.Ridhiwani Kikwete amewaongoza washiriki 1450 katika mbio za hisani za kumbukizi ya miaka 25 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl Nyerere zilizoanzia eneo la Igoma hadi Kisesa Mkoani Mwanza.
Akizungumza na washiriki hao leo Oktoba 12,2024 mara baada ya kuhitimishwa kwa mbio hizo,Kikwete amewapongeza Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza pamoja na Shirika la Utangazaji TBC ambao wamebuni mpango huo ambao unaonesha Urathi wa Mwl Nyerere.
"Baba wa Taifa enzi za uhai wake aliwapigania watanzania kuepukana maadui watatu wa maendeleo ambao ni ujinga,maradhi na umasikini,hivyo leo tunamenzi kwa vitendo kwa mbio hizo zenye kuimarisha afya zetu",Mhe.Kikwete
Amesema licha ya kuimarisha afya zetu lakini zimeimarisha undugu na mshikamano miongoni mwetu kutokana na washiriki kutoka maeneo mbalimbali ya nchini kwetu.
Akitoa hotuba fupi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri Patrobas Katambi,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Said Mtanda amebainisha mwitikio mkubwa walioonesha washiriki wa mbio hizo ni ishara kwamba wamehamasika vya kutosha na ushiriki pia wa kilele cha Mwenge wa Uhuru siku ya Oktoba 14,2024.
"Mhe.Waziri Mwanza hatuna jambo dogo umeshuhudia wiki ya vijana tulivyojipanga vizuri pamoja na hii ambavyo vyote ni sehemu ya kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru na sasa tunakwenda kumuheshimisha Mhe.Rais kwa kujaa uwanjani CCM Kirumba,"Mkuu wa Mkoa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji TBC Dkt.Ayub Rioba amesema mpango uliopo sasa ni kila kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru kutakuwepo na mbio hizo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.