Mhe. Januari Makamba (MB) Waziri wa Nishati leo Julai 14, 2022 amefika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza akiwa kwenye ziara ya Kikazi Wilayani Sengerema kutembelea na kuwasha Umeme kwenye Shule ya Kuzungwangoma ya Watoto wenye Mahitaji Maalum kupitia mradi wa REA III mzunguko wa II.
Mhe. Waziri Makamba amewasifu TANESCO na REA kwa ubunifu wa kuendeleza Miradi ya Gridi Imara na Gridi Mapato iliyofanikisha miradi mikubwa ya kimkakati huku akitolea mfano mradi wa umeme mkubwa kwenye viwanda wilayani Mkuranga ambavyo sasa vinazalisha na kuipatia fedha nyingi serikali.
"Mhe. Mkuu wa Mkoa, tembeeni kifua mbele mkijiamini maana Wakandarasi wapo kazini na mikataba imesainiwa hivyo sasa hakutakua na tatizo la umeme na tumekwamua miradi iliyokua ikisuasua na kwa sasa tumeamua kuajiri vijana kwenye kila wilaya ambao watakua kiungo cha taarifa kwa viongozi kwenye wilaya kwa masuala ya REA." Waziri Makamba.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Mhandisi Robert Gabriel amempongeza Waziri Makamba kwa kazi nzuri huku akibainisha kuwa Miradi ya Umeme Mkoani humo inaendelea vizuri huku akitolea mfano Mradi wa umeme wa Nyamadoke unaokwenda vizuri ikiwa ni mafanikio ya uhodari wake katika kuiongoza wizara.
Kwa upande wake Mbunge wa Sengerema, Mhe. Hamis Tabasamu amemshukuru Waziri Makamba kwa ziara yake ambayo inakwenda kujibu na kitatua kero za umeme hasa kwa wananchi zaidi ya elfu 60 wanaoishi kwenye kisiwa cha Chimfufu
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.