Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (MB) leo tarehe 05 Desemba, 2025 amewasili Mkoani Mwanza na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Said Mtanda ambapo anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi.

Dkt. Nchemba anatarajiwa kufanya ziara ya siku moja ya ukaguzi wa madhara yaliyosababishwa na Vurugu zilizotokea siku ya Uchaguzi Mkuu tarehe 29 Oktoba, 2025 pamoja na kuzungumza na wananchi katika uwanja wa Nyamagana.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.