Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (MB) mapema leo ijumaa tarehe 23 Januari, 2026 amewasili Mkoani Mwanza na kupokelewa na Mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Said Mtanda.

Mhe. Waziri Mkuu anatarajiwa kufanya ziara ya Kikazi ya siku moja ambapo atakagua mradi wa ujenzi wa kituo cha kuratibu ufuatiliaji na uokozi katika ukanda wa ziwa Victoria katika eneo la Uwanja wa Ndege wa Mwanza wilayani Ilemela.

Vilevile, Mhe. Waziri Mkuu ataweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa matenki, vituo vya kusukuma maji na mabomba makuu katika Mtaa wa Sahwa kata ya Lwahnima Jijini Mwanza kabla ya kuhitimisha ziara kwa Kuzindua meli ya kisasa ya MV. New Mwanza katika bandari ya Mwanza Kusini.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.