Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Adam Malima amewakaribisha wananchi waliopo Mikoa jirani siku ya kesho kujitokeza kumpokea Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kasim Majaliwa Majaliwa(MB) anayekuja kufungua kongamano la Wachimba Madini wadogo na kutembelea mabanda ya maonyesho ya shughuli hizo kwenye viwanja vya Rock City Mall.
Akizungumza leo katika Mkutano na Vyombo vya Habari,Mkuu huyo wa Mkoa amesema ziara hiyo ya siku moja ya Mhe.Waziri Mkuu,imewajumuisha kwenye kongamano hilo wadau wa Sekta ya Madini wapatao 1400.
"Hii ni fursa ya kipekee kwa Mkoa wetu kupata nafasi hii,wiki ya Madini inafanyika kwa mara ya kwanza chini ya Shirikisho la Vyama vya Wachimba madini wadogo FEMATA naamini elimu na majadiliano mbalimbali yatakayofanyika yataleta tija na kukuza uchumi wa nchi",Mhe. Malima.
Amesema Mkoa wa Mwanza unafarijika kwa kufanyika kongamano hilo na wiki ya Madini kwani baadhi ya Wilaya kama Misungwi,Sengerema na Kwimba zipo shughuli za kuchimbwa baadhi ya madini hivyo,wahusika watanufaika kwa namna moja au nyingine.
"Serikali imeweka mazingira mazuri kwa wachimbaji wadogo na hadi sasa zimetumika sh.Bilioni 145 kama mikopo kutoka Taasisi za kifedha ambapo hapo awali wachimbaji wadogo walikuwa wakihofiwa kupewa mikopo",Mhe.Dkt.Steven Kiruswa,Naibu Waziri wa Madini.
"Tumezidi kupiga hatua tofauti na hapo awali,tunafurahia kuwa na Serikali sikivu changamoto zetu nyingi zimefanyiwa kazi na sasa tunaendesha shughuli zetu kwa kujiamini na kulipa kodi," John Banna,Rais wa FEMATA.
Awali kabla ya Mkutano huo na Vyombo vya Habari Mhe.Malima,Kamati ya Usalama ya Mkoa pamoja,Naibu Waziri wa Madini na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela wamefanya ukaguzi wa mabanda ya maonyesho ya Madini yaliyopo kwenye viwanja vya Rock City Mall.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.