Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo (Mb) amezungumza na wakuu wa Mikoa na Wilaya kwa njia ya "Video Conference" leo tarehe 23/10/2019 moja kwa moja akiwa Dodoma.
Lengo la mkutano ilikuwa ni kutoa maelekezo mbalimbali kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta za Afya,Elimu miundombinu pamoja na ukusanyaji wa mapato.
Katika sekta ya afya amepokea taarifa kutoka kwa Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa kuhusu ujenzi wa hospitali za wilaya na vituo vya afya vilivyopatiwa fedha na Serikali na maendeleo ya ujenzi yaliyofikiwa sasa.
Aidha katika Sekta ya Elimu taarifa ya hali ya ukarabati wa shule kongwe na ujenzi wa vyumba vya madarasa imetolewa.
Mhe.Jafo amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella kwa utekelezaji wa miradi ya afya kwa kiwango kikubwa na kutaka mikoa mingine kuiga mfano huo.
" Nakupongeza sana Mhe.Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa uhamasishaji mkubwa wa uandikishaji wa orodha ya wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 kwani Mwanza mmefanya vizuri sana," alisema Jafo.
Aidha, Mhe. Jafo ametoa maelekezo kuwa Viongozi wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha kuwa ukusanyaji wa mapato kwenye Halmashauri zote unasimamiwa kikamilifu, pia kuhamasisha wananchi kujitokeza kupiga kura kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 24/11/2019 na kuwataka viongozi kuhakikisha wanafunzi wote watakaochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza wanajiunga na masomo ya Sekondari na kuhakikisha uwepo wa miundombinu kwa ajili hiyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.