Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe. Jenista Mhagama ameiagiza bodi ya Watumishi Housing (WHC) kufanya tathmini ya gharama za Mradi wa Nyumba za Kisesa Mjini Mwanza ili kuona namna ya kupunguza gharama za Uuzaji na upangishaji kulingana na maisha halisi ya Watumishi wa Umma.
Ametoa agizo hilo leo mchana tarehe 22 februari, 2023 alipotembelea Mradi wa Nyumba za Watumishi Housing uliopo kwenye eneo la Kisesa Magu-Mwanza wenye nyumba 59 zilizojengwa kwa Shilingi Bilioni 3.93 ambazo zinauzwa na kupangishwa.
"Ni nyumba nzuri, zinakalika ila shida ni gharama ya upangishaji na kuuzia kuwa kubwa na hali hiyo imetokana na gharama ya Mkandarasi aliyetekeleza mradi huu sasa nawaomba nendeni mkakae na bodi mkafanye tathmini ili mfanye tathmini na kushusha bei bila kuleta hasara hiyo itatusaidia kupata wapangaji na wanunuzi watakaotokana na wapangaji hao." Mhe. Mhagama.
Aidha, amewatala watendaji wa shirika hilo kutoa Elimu kwa watumishi na wananchi juu ya bidhaa zote zinazopatikana kwenye shirika hilo kama vile 'Mfuko wa Faida' ili wananchi wajiunge na kuwa wawekezaji na kuweza kunufaika na mfuko huo.
Naye, Mkuu wa wilaya ya Magu Mhe. Rachel Kasanda amewashukuru Shirika la Watumishi Housing kwa kuwapatia Wananchi Makazi bora na kusaidia kupanua mji tofauti na siku za awali ambapo eneo hilo lilikua na thamani ya chini tofauti na sasa ambao limekua na kuongezeka kwa wawakezaji kutokana na fursa zilizopo.
"Mfuko wa nyumba ni Mfuko wa Faida ambao unasaidia wananchi kuwekeza fedha kwa pamoja na Watumishi Housing inamfanya kuwa mwekezaji na anaanza na Tshs elfu 10 au zaidi ambapo uwekezaji huo ni rahisi kwani unatumia njia ya simu janja hadi unakua mwekezaji." Amesema Dkt. Fred Msemwa, Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Imvestiment.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.