Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima amezitaka Halmashauri mkoani humo kuwa wabunifu kwenye ukusanyaji wa Mapato ya ndani ili waweze kuongeza uwezo wa kujiendesha.
Amesema hayo leo (Januari 15, 2023) wakati wa kikao kazi cha pamoja na Halmashauri ya Kwimba kilichojadili kuhusu vigezo muhimu vya kuzingatia katika maandalizi ya bajeti ya mwaka 2023/24.
Malima amesema uhai wa Halmashauri yoyote hutegemea sana makusanyo ili kukidhi Utekelezaji wa shughuli za kila siku kupitia bajeti zilizopangwa na kwa mujibu wa sheria hivyo ni wanapaswa kuwa na mpango wa kukusanya mapato mengi zaidi.
"Kwa jinsi nilivyowasikiliza nimebaini mna vyanzo vizuri sana vya mapato na mnaweza kukusanya zaidi hata ya Bilioni Tano na wala sio kama mlivyokadiria wenyewe kufikia kwenye Bilioni 3.1 huu ni uoga wenu tu na bora mngekadiria fedha nyingi ili mjitume zaidi" Malima.
Naye, Katibu Tawala Mkoa Balandya Elikana ameziagiza Halmashauri kuweka kumbukumbu za vyanzo vya mapato ambayo viña mwendelezo wa kufanya vizuri na ambavyo havifanyi ili kuwa na dira ya wapi pa kupita katika kuhakikisha Halmashauri inafanya vizuri kwenye ukusanyaji.
"Hadi mwezi huu ambapo tumebakisha miezi mitano kumaliza mwaka mmeshakusanya Bilioni 1.7 ambayo ni zaidi ya asilimia 85 ya mlichojipangia na tuna miaka mitatu mfululizo tunavuka malengo, hii maana yake ni kwamba hatuko sawa katika kukadiria mapato ya ndani na tujue ya kwamba tunapokadiria chini maana yake tunakaribisha matumizi mabaya ya fedha." Balandya Elikana.
Akitoa taarifa ya Halmashauri, Mkurugenzi Mtendaji Happiness Msanga amefafanua kuwa kwa mwaka 2023/24 wamekadiria kukusanya zaidi ya Bilioni 3.3 wakati kwa mwaka wa fedha unaoendelea wamekusanya Bilioni 2.46 ambayo ni sawa na asimilia zaidi ya 85.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.