WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI KUTOKOMEZA UVUVI HARAMU ZIWA VICTORIA
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (MB) amesema Serikali inaweka mikakati maalum kwa ajili ya kutokomeza na kupambana na uvuvi haramu katika ziwa Victoria ambazo zitasaidia katika kuzilinda rasilimali.
Amesema hayo wakati akizungumza na wadau wa uvuvi kutoka katika Mikoa ya kanda ya ziwa leo Oktoba 8, 2024 katika Ukumbi wa Nyakahoja Mkoani Mwanza.
Mhe. Ulega amewataka wavuvi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Serikali ili kuweza kutokomeza uvuvi haramu na kusaidia katika upatikanaji wa malighafi katika viwanda vya samaki na kukuza ustawi wa sekta ya uvuvi.
Sambamba na hayo Mhe. Ulenga ametoa rai kwa wadau wa uvuvi kutoka katika Mikoa ya kanda ya ziwa kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika vikao na mikutano inayohusiana na maswala ya uvuvi kwakua maoni na mawazo yao yanamchango mkubwa Serikalini.
"Nyinyi ambao ndiyo wadau wenyewe mnaweza mkachukua kwa wepesi lakini nawaambieni kwa upande wa Serikali mnachukuliwa kwa uzito na ndiyo maana wakifanya maamuzi lazima watasema tulikaa na wadau". Amesema Mhe. Ulega.
Naye Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ndg. Patrick Karangwa akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala amesema Mkoa unaendelea kusimamia rasilimali na uhifadhi wa ziwa Victoria kwa ustawi wa uchumi wa Taifa na wananchi.
"Mkoa unaendelea kusimamia utekelezaji kwa lengo la kulinda rasilimali za uvuvi katika ziwa Victoria ili kuweza kuwanufaisha wananchi na Taifa kwa ujumla". Amesema kawamba
Nao baadhi ya washiriki wa kikao hicho wameiomba Wizara ya mifungo na Uvuvi kuwapatia vifaa vya kutosha Maafisa uvuvi ili kuwawezeshe kufanya kazi kwa wakati wote na kuhakikisha wanatokomeza uvuvi haram katika ziwa Victoria in.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.