Wizara za TAMISEMl, Afya zafanya ziara ya Uhimarishaji mifumo Mwanza
Mkurugenzi wa Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe -TAMISEMl Dkt. Ntuli Kapologwe ametoa wito kwa watumishi wa Sekta ya Afya kuwahudumia wananchi kwa dhati na kiweledi ili jamii iweze kulindwa na kujenga uaminifu zaidi kwa kada hiyo nchini.
Amesema hayo leo Agosti 10, 2023 wakati akizungumza na Watumishi na wadau wa Sekta hiyo kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Mwanza wakati wa Kikao cha Majumuisho ya ziara ya Uhimarishaji mifumo na kujenga uwezo kwa watumishi wa sekta hiyo akiongozana na Ujumbe kutoka Wizara ya Afya.
"Shabaha ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ni kuboresha huduma kwa wananchi hivyo sote tukijituma kufanya kazi tutasaidia kufikia lengo hilo kwani fedha zimeletwa nyingi sana hivyo ni lazima zilete matokeo chanya kwa wananchi." Dkt. Kapologwe.
Aidha, amewataka wasimamizi na Wadau wa Afya nchini kuhimarisha mifumo ya afya hususani kwa kuhakikisha wanaboresha huduma za rufaa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili kujenga jamii yenye afya bora kutokana na huduma bunifu na bobezi.
"Ziara yetu inalenga kuimarisha mifumo ya afya na kujengeana uwezo kwenye namna ya kutoa huduma za afya kwa kuziangalua changamoto na mafanikio kwenye Maeneo mbalimbali ili kuona namna bora ya kuboresha." Amesisitiza.
Naye, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Thomas Rutachunzibwa ameomba Wizara za Afya na TAMISEMl kuboresha huduma huku akibainisha baadhi ya changamoto zinazoikabili Sekta hiyo kama upungufu wa watumishi, kutokuwepo kwa wataalamu wa lugha ya Alama kwenye vituo vya kutolea huduma kwa ajili ya wenye Ulemavu.
Vilevile, ametoa ombi kwa wizara kuona namna ya kuingiza bidhaa za wajawazito kwenye miradi ili isaidie kuwafikia kwa urahisi walengwa na pia ametoa pendekezo kwa wizara za kisekta kuweka utaratibu utakaosaidia wananchi wenye madimbwi kupata dawa za viuadudu kwa gharama ndogo wakati Idara hiyo ikiendelea kutoa msaada wa kitaalam kwenye matumizi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.