Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella amepokea Kemikali bashilifu lita 92.226 aina ya Ethyl Alcohol kutoka kwa Mhakiki mali Mkoa wa mwanza Bw.Colman Shayo ili zitumike katika kutengeneza vitakasa mikono kwa ajili ya kujikinga na maambukizi yatokanayo na virusi vya corona baada ya taratibu na kesi kuamriwa na kukabidhiwa kwa serikali.
Akielezea kuhusiana na Kemikali hizo Kaimu Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na madawa ya kulevya Bw. James Kaji alisema Kemikali hizo zilikamatwa baada ya kuingizwa nchini bila kufuata utaratinu kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali baada ya kupelekwa Mahakamani na kesi kuamuliwa zilitaifishwa na Serikali.
"Tumeamua tuukabidhi Mkoa, hii ni kutokana na juhudi za Mhe.John Mongella Mkuu wetu wa Mkoa katika kupambama na janga la corona kwa jitihada alizozifanya kuonana na ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Kamati inayoshughulika na kudhibiti maambukizi ili zitumike kutengeneza vitakasa mikono,"alisema Kaji.
Akiongea kwa niaba ya Mkemia Mkuu wa Serikali Bw. Bonventura Masamba amesema wamepokea mapipa mia tatu sitini na saba (367) yenye ujazo wa lita mia mbili hamsini (250) kila moja na kufanya jumla ya lita iahirini na moja elfu na mia tisa sabini na sita(21,976)yenye kemikali aina ya Ethin alcohol yaliyokamatwa disemba 2017 katika keai za jinai 195 na 197 za 2018.
"Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ni taasisi ambayo pamoja na majukumu mengine iliyopangiwa na Serikali ni kusimamia uingizwaji,usafirishwaji na kudhibiti namna bora ya matumizi ya kemikali,"alisema Masamba.
Akikabidhi mali hizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella Bw.Colman Shayo ambaye ni Mhakiki Mali wa Mkoa wa Mwanza amesema atashirikiana na Mkoa ili kuhakikisha kuwa mali hizo zinatumika kwa lengo lililokusudiwa na kuhakikisha wanatekeleza wajibu huo kwa uadilifu na utaratibu unaokubalika na Serikali.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella amesema katika vita dhidi ya kupambana na madawa ya kulevya vyombo vyetu vya ulinzi na usalama waliaimamia kikamilifu na ndiyo imepelekea kupatikana kwa kemikali hizo bashilifu.
"Tumepokea maelekezo kutoka ofisi ya Waziri Mkuu na sisi hapa tunachofanya baada ya wenzetu kutoka Dodoma na Dar es Saalam ni kupokea kubwa ni kwamba tunaahidi kuaimamia kwa uadilifu na weredi kazi hiyo ya kutengeneza vitakasa mikono na kuhakikisha kwamba kemikali hizi hazirudi tena sokoni maana yake tayari ziliishakamatwa,"alisema Mhe.Mongella.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.