Zingatieni Mafunzo kuepusha Serikali kuchukiwa na kuingia gharama za kisheria: Katibu Mkuu Ikulu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu Mululi Mahendeka leo Januari 22, 2024 amefungua mafunzo ya Uzingatiaji Sheria, Kanuni na taratibu za utumishi wa Umma kwa Makatibu Tawala Wasaidizi, utawala na Rasilimali watu kutoka Mikoa ya kanda ya ziwa na kuwataka kuzingatia mafunzo hayo ili kuwepo na tija katika utoaji huduma kwa watumishi na wananchi.
Mahendeka amesema kutokana na kutoelewa kwa miongozo ya sheria imechangia kuwepo na mlolongo wa malalamiko kutoka kwa watumishi na wananchi yanayowafika viongozi wa juu hali ambayo imechangia kuzorotesha utendaji kazi wa Taifa kwa ujumla.
"Ndugu washiriki wa mafunzo haya ambao wengi wenu ni watumishi wenzangu,Ofisi ya Rais imeingia gharama ya kuandaa mafunzo haya kwa siku 5 ikitambua umuhimu wake,mkizingatia ipasavyo sheria,kanuni na taratibu mtaepusha Serikali kuchukiwa na kuingia gharama zinazotokana na mashauri yaliyotokana wahusika mliopewa dhamana ya kusimamia kushindwa kuwajibika kikamilifu,"Katibu mkuu Ikulu.
Amebainisha hakuna sababu ya kuwapa kazi ya kutatua kero wa za wananchi na watumishi viongozi wetu wa juu akiwemo Rais,Makamu wa Rais,Waziri Mkuu au Katibu mkuu kiongozi wakati waliopewa jukumu hilo wapo lakini wameshindwa kutimiza wajibu wao.
"Kushindwa kutafsiri vizuri sheria,kanuni na taratibu imechangia watumishi kutumia muda mwingi kwenye vyombo vya kisheria kusaka haki yao na kushinda mashauri yao na mwishowe Serikali kuingia gharama," Xaveri Daud Naibu Katibu mkuu OR-Menejimenti ya utumishi wa umma
Mwenyeji wa mafunzo hayo ambaye ni Katibu Tawala mkoa wa Mwanza Ndg.Balandya Elikana ameishukuru Ofisi ya Rais kwa kuyaleta mafunzo hayo Mkoani humo na kuwataka washiriki wote kuja na matokeo chanya baada ya kuelimishwa vyema.
"Tunapotoa huduma bora kwa wananchi na watumishi Imani kutoka kwao inazidi kuongezeka kwa Serikali hali itakayo kuwa na tija katika utendaji kazi kwa ujumla," Katibu Tawala mkoa.
Washiriki wengine katika mafunzo hayo wanatoka kwenye Taasisi za Serikali wataalamu wa sheria na Rasilimali watu kutoka mikoa ya Shinyanga,Mara,Geita,Simiyu,Mara,Kagera na Mwanza.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.