Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ametoa wito kwa wakulima mkoani humo kutumia fursa ya uwepo wa mfumo wa stakabadhi za ghala kwa ajili ya kupata uhakika wa masoko na hususani kukuza uchumi wao.

Ametoa wito huo leo tarehe 30 Januari, 2026 wakati akifunga mafunzo ya siku tano kwa washiriki 111 ambao ni mameneja wa maghala ya mazao na watunza kumbukumbu yaliyoratibiwa na Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za ghala katika kuelekea msimu wa zao la Choroko 2026/27.

Mhe. Amesema serikali imeweka mfumo rasmi wa kusajili wakulima nchini na mazao wanayolima ili kujua ni mazao gani yanazalishwa kwa wingi na hali ya masoko na kuhakikisha inaleta mageuzi kwenye sekta ya kilimo.

Aidha, amewataka wasimamizi wa mfumo huo kuhakikisha wanatunza kumbukumbu vizuri kwa kuwaingiza kwenye kanzidata wakulima wote na hali ya uzalishaji wao ili kupata msingi wa namna ya kutafuta masoko kwani kutanua na taarifa za eneo linalolimwa na hali ya uzalishaji.

“Tamaa ni mbaya na haiwezi kumsaidia kijana yeyote, tufanye kwa kuzingatia sheria na taratibu za nchi ili kusogeza mbele sekta ya kilimo na uzalishaji kwa ujumla, twendeni tukawasaidie wakulima kwa uzalendo.” Mhe. Manda.

Ametoa wito kwa vijana kutumia maarifa waliyoyapata kwenye vyuo kuleta mabadiriko chanya katika jamii kwa kuyatumia kwa manufaa ya wengine waliokosa elimu ambao wanawaangalia wasomi kama kioo kwao na wakafanye hayo kwa uadilifu.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.