Naibu waziri wa kilimo Mhe. Dkt Mary Mwanjelwa amezindua maonesho ya wakulima (nanenane) katika kanda ya ziwa magharibi inayojumuisha Mwanza,Geita,Kagera katika viwanja cha Nyamongolo, ambapo maonyesho hayo yamehudhururiwa na wadau wapatao 330 wakubwa, wa kati 80, wadogo 250 na Mamlaka za Serikali za Mitaa 12.
Mhe. Dkt.Mwanjelwa amesema kuwa wadau hao wanajumuisha Taasisi za Umma,Taasisi za Utafiti, Taasisi za Elimu, Taasisi za Fedha, Makampuni ya Zana za kilimo na Pembejeo, Bodi mbalimbali za Mazao, Wakulima na Wafugaji,wasindikaji wa mazao mbalimbali, makampuni ya mawasiliano, na makampuni ya vinywaji.
Aidha kaulimbiu ya mwaka huu inasema kuwa“Wekeza katika kilimo,Mifugo na Uvuvi kwa maendeleo ya viwanda” hivyo Mhe. Mwanjelwa amesisitiza kwa wah.Wakuu wa wilaya pamoja na Maafisa Ugani kufanya kazi ya kutoa elimu kwa wananchi ili kukuza maendeleo ya kilimo cha biashara.
“Changamkieni fursa ya kilimo kwani ni maisha, kilimo kinasaidia kupunguza umaskini na tutakuza uchumi na biashara hivyo tutaimarisha,tutafufua na kuboresha vyama vya ushirika ili kuweza kuwakomboa wakulima,”alisema Mwanjelwa.
Naye Meneja wa kanda George Upina anayejishughulisha na kilimo cha kisasa amesema kuwa kilimo hiki hakijali msimu na kinazalisha mazao mengi kwa muda mfupi na kinalimwa popote itolewe elimu ili kuinua kilimo cha biashara na kukuza teknolojia katika kilimo.
Hta hivyo Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema kuwa atatoa vyeti kwa washiriki wote walioshiriki katika sherehe ya nanenane na kuwazawadia washiriki watakao fanya vizuri zaidi siku ya kilele cha maonesho ya sherehe za nanenane tarehe 08.08.2018
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.