Asilimia 48 ya wanawake wanaobeba ujauzito mara kwa mara( wenye nzao nyingi) walipoteza maisha mwaka jana wakati wa kujifungua mkoani Mwanza.
Aidha ,Wilaya ya Ukerewe mkoani humo mwaka jana iliongoza kwa wanawake kufuata uzazi wa mpango kwa asilimia 48 ikifuatiwa na Mwanza jiji asilimia 43, huku Ilemela ikishika nafasi ya tatu kwa asilimia 42.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Mwanza na Mratibu Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto mkoani Mwanza, Secilia Mrema alipozungumza na mwandishi wa habari hii ofisini kwake.
Alisema kiwango kidogo cha matumizi ya uzazi wa mpango kimechangia vifo vya wazazi na watoto wachanga hasa wanawake wanaozaa mara kwa mara.
Akizungumzia masuala ya afya ya uzazi, Secilia alisema kiwango cha matumizi ya uzazi wa mpango kwa mwaka jana kilifikia asilimia 39 kutoka asilimia 18 mwaka 2015.
Secilia alisema kiwango cha uzazi wa mpango kimeongezeka huku vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga vikipungua mkoani humo.
Alisema mafunzo kwa watoa huduma za uzazi wa mpango zimeongezeka kutoka asilimia 35 mwaka 2019 hadi kufikia asilimia 45 kwa mwaka jana.
Kwa upande mwingine,Secilia alisema bado kuna uelewa mdogo kwa wananchi kuhusu uzazi wa mpango pamoja na upungufu wa watumishi wenye ujuzi wa kutoa huduma za afya.
Aidha, alisema sekta hiyo bado inakabiliwa na upungufu wa vifaa vya kutoa huduma za uzazi wa mpango ikiwamo (IUCD kits)pamoja na kukabiliwa na uhaba wa watumishi wenye ujuzi wa kutoa njia za uzazi wa mpango baada ya kujifungua.
Kwa upande wake, Ofisa Mahusiano wa Kanda ya Ziwa wa shirika la Marie Stopes Tanzania, Shamim Abdallah alisema wanafanya kazi kwa ushirikiano na mkoani Mwanza, lengo likiwa ni kutoa elimu, kufundisha watoa huduma ili kuwafikia watu wengi husani wananchi wanaoishi visiwani.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.