• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Majaliwa Amaliza Tatizo la bei ya Pamba

Posted on: May 29th, 2019


Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ameumaliza mgogoro wa bei uliokuwepo baina ya wakulima wa zao la pamba nchini na wanunuzi, ambapo sasa zao la pamba litaendelea kununuliwa kwa bei elekezi ya serikali ya sh. 1,200 kwa kilo.

Waziri Mkuu aliumaliza mgogoro huo  mara baada ya kukutana na makundi ya wanunuzi na wakulima, wakuu wa mikoa/wilaya na wakurugenzi watendaji kutoka kwenye mikoa inayolima pamba nchini wakati wa mkutano wa dharula wa wadau wa tasnia ya pamba nchini.

Alisema katika kukithamini kilimo cha pamba, Serikali iliitisha vikao vingi tangu mwaka jana kwa ajili ya kuimarisha zao hilo na kwamba dhamira yake ni kuona kilimo cha pamba kinamnufaisha mkulima.


Alisema hatua hio  imeleta mafanikio ya uzalishaji wa zao hilo kutoka tani 222,000 kwa msimu uliopita wa kilimo hadi kufikia karibu tani 450,000 kwa msimu wa mwaka huu na aliwahakikishia wakulima kuwa pamba yote iliyozalishwa kwa msimu huu itanunuliwa yote.


Aliwataka wakuu wa mikoa na wilaya, wakurugenzi watendaji kwenye maeneo kuangalia utaratibu mzuri wa kuwasaidia wanunuzi ili kuhakikisha pamba yote inayonunuliwa kutoka kwa mkulima inawafikia salama.

“ Aidha muweze kujiridhisha na mifumo ya fedha iliyopo kama iko sawa ili wakulima wetu waweze kulipwa fedha zao kupitia benki, alisema na kuwashukuru wanunuzi wa pamba kwa kuitikia mwito wa serikali kwa kununua pamba kwa bei elekezi ya serikali.


Aliziagiza Kamati za ulinzi na usalama za wilaya na mkoa kuwahakikishia wanunuzi na wakulima usalama wa fedha zao mara baada ya kuuza na kununua pamba ili kuhakikisha pande zote mbili zinakuwa salama.


“Lengo letu kama serikali kama serikali ni kuhakikisha mwenendo wa manunuzi unakwenda vizuri,” alisema na kuwahakikishia wanunuzi kuwa biashara yao itasimamiwa vizuri.


Kwa upande wa ubora wa pamba, alisema mkakati uliopo wa serikali kwa sasa ni kuhakikisha kuwa inaimarisha ubora wa zao la pamba kwa kuwawezesha wakulima kulima kilimo chenye tija kwenye maeneo yao.


Alisema mkakati huo utakwenda sanjari na viongozi na watalaam wa zao hilo kuwaelimisha wakulima juu ya ubora wa zao hilo ili hata baada ya mavuno, wasichanganye maji na mchanga kwa ajili ya kuongeza uzito ili kujipatia fedha, jambo ambalo litasababisha bei ya pamba kushuka kwenye soko la dunia.


“ Pamba kukosa ubora, wakati mwingine unasababishwa na wakulima kukosa sehemu ya kuhifadhia pamba yao, niwaombe viongozi mjiridhishe kwenye maeneo yenu kama pamba ina ubora unaotakiwa,” alisema na kuwataka viongozi kuzihakiki mizani zinazotumika kununulia pamba ili kubaini zenye kasoro na hatua zichukuliwe kwa wanunuzi wenye mizani za kumpunja mkulima.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.