• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Mwanza yaadhimisha siku ya Kitaifa ya maandishi ya Braille kwa kukabidhi fimbo nyeupe 150

Posted on: February 23rd, 2023


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Adam Malima amewataka wazazi kutokuficha na kunyanyapa watu wenye ulemavu na kutoa angalizo kuwa kila mtoto ana kipaji chake.

Akizungumza leo februari 23, 2023 katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza ambapo maadhimisho hayo yamefanyika Kitaifa Mhe.Malima amesema Serikali ya awamu ya 6 chini ya Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutambua umuhimu wa watu wenye ulemavu imezindua Mwongozo wa Taifa wa Utambuzi wa Mapema na Afua Stahiki kwa watoto wenye ulemavu wa mwaka 2021,pia Mwongozo wa Utekelezaji, Ujumuishwaji na Uimarishaji wa huduma kwa watu wenye ulemavu wa mwaka 2022.

"Serikali kwa mwaka 2022,imeandikisha watoto 2,883 katika elimu ya swali ambapo wasichana 1,413 na wavulana 1,470, wakati Shule ya Msingi 3,318 na MEMKWA 122," amesema Mhe.Malima.

Hata hivyo amesisitiza kuwa Serikali imeajili Kada ya walimu nafasi 9800 na kada za afya 7612 ambapo jumla ya watu wenye ulemavu 261 sawa na asilimia 2.7 walikidhi vigezo na kupata ajira ya ualimu ambapo kati ya hao 261ya watu wasioona walikuwa 61.

Mwakilishi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu  Joy Maongezi amesema Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na wadau imetoa Fimbo nyeupe 35, viti mwendo 35 na mafuta kinga 35 pamoja na miwani kwa wanafunzi 174, Essilor  glasses 174,miwani yenye lenzi inayobadilika kulingana na mionzi ya jua 172, monocular 268, makasha ya miwani 183, mabegi 341 pamoja na viungo bandia kwa watu 179 vyenye thamani ya shilingi 118,552,000 kutoka Taasisi ya Lohana.

"Serikali imeendelea kuyapa kipaumbele masuala ya watu wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na masuala ya Elimu, uwezeshwaji wa kiuchumi, afya na ajira," amesema Bi. Maongezi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa maafisa Elimu wa Elimu maalumu Issa Kambi, amesema Maafisa Elimu wa Elimu maalum ndiyo kiini cha maandishi ya Braille na ameahidi kuendelea kujitoa kwa hali na mali katika kusimamia elimu kwa wanafunzi wasio na usoni.


Akisoma risala kwa niaba ya Wasioona kwa  mgeni rasmi, Mshauri wa Jumuiya ya Maendeleo ya  wasioona  Tanzania James Shing'wenye amesema anashukuru Serikali kwa kuja na wazo la bima ya afya kwa wote kwani wengi wa wenye ulemavu hawana uwezo wa kugharamia matibabu hivyo bima ya afya ni ukombozi kwa wote.

"Tunaiomba serikali iweke mifumo mizuri ya Usalama katika miundombinu ya mashuleni na maeneo ambayo wasioona wanapatia huduma, walimu wa elimu maalum waongezwe pamoja na kupatiwa motisha," amesema Shing'wenye.

Aidha, ameiomba Serikali kuongeza vyuo vya walimu wa elimu maalum na motisha, pia iboreshe mazingira na mahitaji kwa wanafunzi wasioona pamoja na mashine za kidijitali za kuandikia.

Pamoja na hayo, Shing'wenye  ameiomba serikali kutenga bajeti maalumu ya maadhimisho ya kila mwaka kwa ajili ya wasioona pamoja na kuanzisha mpango maalumu wa bima ya afya kwa watu wasioona.


Naye, Mwenyekiti wa chama cha wasioona Tanzania Omar Itambu   amesema kwa hapa Tanzania 1960 maandishi ya Braille yalianzia Shule ya Msingi  Buigiri  huko Dodoma na imekuwa ni ukombozi mkubwa kwa wasioona kwani hata yeye mwenyekiti amesoma kupitia maandishi haya ya Braille.

"Niwaase wazazi wote ukipata mtoto mwenye ulemavu wowote ule, mpeleke Shule siku hizi hakuna kinachoshindikana,"amesema Itambu.

"Sasa hivi Serikali inatujali sana, japokuwa changamoto haziishii.....hivyo tunaiomba serikali kuingia kwenye mfumo wa dijito Braille  ambao utapunguza ama kumaliza changamoto za wasioona," amesisitiza.

Siku ya Kimataifa ya maandishi ya Braille huadhimishwa kote duniani tarehe 4 Januari ya kila mwaka, kwa mwaka huu yamebeba Kauli mbiu ya "Eneza Ufahamu Kuhusu Umuhimu wa Braille."

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.