RC MAKALLA AAGIZA KUKOMESHWA KWA UVUVI HARAMU ZIWA VIKTORIA
*Ataka kukomeshwa kwa uvu
*Ataka viongozi kudhibiti Uhamiaji haramu hususani kwenye visiwa*
*Aagiza kurudishwa kwa Mkandarasi aliyejenga barabara Nansio ambayo imebainika kuwa na kasoro*
*Amesisitiza nidhamu kazini pamoja na kushirikiana*
*Awataka Ukerewe kutunza miradi ya kimkakati*
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, CPA Amos Makalla leo Juni 06, 2023 amefika Kisiwani Ukerewe akiwa katika Muendelezo wa ziara yake ya kikazi ya kujitambulisha akihakikisha anafika na kuzungumza na Viongozi na Watendaji katika Halmashauri zote za Mkoa huo.
Akizungumza wilayani Ukerewe, Mhe. Makalla ametoa wito kwa wanachi wa Ukerewe kuhakikisha wanafanya shughuli za uvuvi kwa mujibu wa sheria na sio kwa kuharibu mazalia ya samaki aidha ametoa wito kwa Kamati ya Usalama kusimamia hilo wakati wote ili kuimarisha uchumi wa jamii kupitia shughuli za uvuvi.
"Nafahamu ya kwamba Uvuvi ndio shughuli yetu kuu hapa lakini nimekuja kuwakumbusha kuvua kwa kuzingatia sheri tusitumie mabomu, nyavu haramu na aina yoyote ya Uvuvi haramu ili samaki waendelee kuzaliana kwani huo ndio uchumi wetu hivyo tukiharibu tutaharib uchumi wetu." Mhe. Makalla.
Aidha, ameiagiza idara ya Uhamiaji kushirikiana na wananchi hususani kwenye visiwa kuhakikisha hakuna Wahamiaji haramu kwani wilaya hiyo imetawanyika sana kijiografia kwa kuzingatia imezungukwa na visiwa 38 vidogo vidogo vikiwemo 15 vyenye makazi ya kudumu.
Vilevile, amemuagiza Mkuu wa Wilaya kwa kushirikiana na Meneja wa TARURA kuhakikisha mkandarasi aliyejenga barabara ya Mjini yenye urefu wa zaidi ya KM 1 kuhakikisha anaifanyia marekebisho kwenye kasoro zilizobainika ili wananchi wapate mradi wenye kiwango kinachokubalika na thamani ya fedha.
"Mhe. Mkuu wa Wilaya shirikiana na wenzako mrudisheni Mkandarasi aliyejenga barabara ya kiwango cha lami hapa mjini ambayo ina kasoro nyingi na kusababisha manung'uniko kwa wanamchi ili aje aifanyie marekebisho kuondoa kasoro hizo," amesisitiza.
Aidha, Mhe. Makalla amesisitiza kufuatwa kwa taratibu za fedha kwa kukusanya na kuwasilishwa benki kabla ya kuzitumia na akawataka watumishi kushirikiana na Mkaguzi wa ndani wa Halmashauri kujibu hoja za Ukaguzi kwa wakati ili kuifanya Halmashauri hiyo kuenenda kisheria.
Aidha, amesisitiza uadilifu kwa watumishi wa umma katika kuwahudumia wananchi na akatoa wito kwa viongozi kushirikiana na watendahi katika kusimamia miradi ya Maendeleo ili kujenga imani kwa wananchi dhidi ya Serikali yao inayoongozw na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mhe. Hassan Bomboko, Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe amesema Wilaya hiyo iliyozungukwa na visiwa 38 vidogo vidogo ambapo 15 vina makaazi ya kudumu watu wake wana amani na wanaendelea na shughuli za kujitafutia ridhiki hususani kwa shughuli za uvuvi kwa amani.
Amesema Serikali kuu imekua ikiwajali sana kwani wamepokea zaidi ya Bilioni 12 ndani ya mwaka huu wa fedha kwa ajili ya kutekeleza Miradi mbalimbali katika Sekta za Nishati, Afya, Elimu, Miundombinu na Maji na kwenye hilo amemshukuru Mhe. Rais Samia kwa niaba ya wananchi wa kisiwa hicho.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.