RC MTANDA AAHIDI USHIRIKIANO ZAIDI JJI LA MWANZA NA TAMPERE-FINLAND
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amempokea Balozi wa Finland nchini Mhe.Theresa Vitting na kumuahidi ushirikiano zaidi katika sekta mbalimbali baina ya Jiji la Mwanza na Tampere ili kuwaletea maendeleo wananchi na kukuza uhusiano huo.
Akizungumza na mgeni wake leo Februari 7, 2025 Ofisini kwake Mkuu huyo wa Mkoa amebainisha nchi ya Finland ni miongoni mwa Mataifa ya mwanzoni kabisa kuingia uhusiano wa kibalozi mara baada ya kupata uhuru mwaka 1961 na kumekuwa na muendelezo mzuri baina ya Mataifa hayo.
"Mwaka 1965 tuliingia rasmi kwenye mahusiano ya kibalozi na Finland,na wamekuwa na mchango mkubwa kwetu katika sekta mbalimbali ikiwemo uchangiaji wa kiwango kikubwa wa bajeti yetu", Mhe. Mtanda.
Amesema kwa upande wa Jiji la Mwanza wamekuwa wanufaika wazuri kwa upande wa Elimu, mazingira na wataalam mbalimbali na pia ametoa fursa kwa Finland kuona uwezekano wa kuwekeza katika ufugaji wa kisasa wa samaki.
"Mwanza asilimia 53 imezungukwa na maji ya ziwa Victoria, Serikali imewekeza kwa vijana kujishughulisha na ufugaji wa kisasa ni fursa nzuri endapo itawapendeza", Mkuu wa mkoa.
Kwa upande wake Mhe,Theresa Vittinng amesema Finland imefurahishwa na matokeo mazuri ya mahusiano na Tanzania na ssa inaangalia namna ya uwekezaji katika madini wakianzia mnyororo wote wa thamani katika utafiti,maabara na kuwajengea uwezo wachimbaji wadogo.
"Leo nipo Mwanza nitakwenda chuo cha ualimu Butimba tunataka kuboresha upande wa michezo,hatulichukulii kama jambo la kufurahisha tu lakini tunatambua umuhimu wake katika Dunia ya sasa",amesisitiza Bi.Theresa
Jiji la Mwanza na Jiji la Tampere kutoka Finland waliingia mahusiano kuanzia mwaka 1988 hadi sasa wakishirikiana mambo mbalimbali ukiwemo usafi wa mazingira
.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.