RC MTANDA AKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO NA KUFUNDISHIA VYENYE THAMANI YA ZAIDI YA MILIONI 36 MISUNGWI
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo tarehe 12 Februari, 2025 amekabidhi vifaa vya kufundishia na michezo vyenye thamani ya zaidi ya Tshs. Milioni 36 kwa shule 3 za Sekondari Wilayani Misungwi vilivyototelewa na Taasisi ya Africa School House.
Akiongea mara baada ya kukabidhi msaada huo katika hafla iliyofanyika katika shule ya sekondari ya Aimee Milembe, Mhe. Mtanda amewashukuru wahisani hao kwa msaada huo muhimu kwa maendeleo ya sekta ya elimu Wilayani humo na Mkoa wa Mwanza kwa ujumla.
"Elimu ndio mtaji mkubwa katika maisha na tunaamini kwenye kuwekeza kwa watoto na katika kufanikisha hilo Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan inatoa fedha nyingi kwenye elimu na tunawashukuru washirika wetu kwa kuwa nasi tangu mwaka 2017 kwa kujenga shule sehemu mbalimbali, nyumba za walimu, visima virefu vha maji." RC Mtanda.
Aidha, Mkuu wa Mkoa amesema ndani ya miaka minne shule mpya 11 za sekondari zimejengwa, mabweni 30, nyumba 12, matundu vya vyoo 133 kwa sekondari na kwamba awali zilikuwepo shule 965 za msingi na sasa 1043 sawa na ongezeko la shule 85 na shule 275 hadi 332 za sekondari sawa na ongezeko la shule 57.
Mhe. Mtanda ameongeza kuwa ndani ya kipindi cha miaka 4 walimu 1168 wameajiriwa na kupangiwa vituo ndani ya Mkoa huo na kwamba Serikali imepata mafanikio kwa kuwa na miundombinu hivyo basi wahisani hao kuunga mkono juhudi hizo ni jambo la msingi sana.
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dkt. Aimee Bessire amesema wanayo furaha kusaidia sekta ya Elimu na siyo tu kwa vifaa hivyo bali wanajenga pia miundombinu kama mabweni, madarasa, vyoo na jiko wilayani humo vinavyogharimu zaidi ya Tshs. milioni 350.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.