Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo Desemba 04, 2025 amefanya ziara katika Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Victoria Nyanza, ambapo amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi pamoja na Wachungaji wa Kanisa hilo ambapo lengo la ziara hiyo ni kuhamasisha amani, utulivu na mshikamano.

Mkuu wa Mkoa amesema ujio wake kanisani hapo ni muendelezo wa kile alichokiita ziara ya amani kuyafikia makundi mbalimbali kupitia Viongozi wao ili nao wakawasilishe ujumbe wa amani na mshikamano kwa wale wanaowaongoza au wafuasi wao.

“Nchi hii ina watu milioni 60, na Mungu anasema hata wakikutanika watu wawili tu wakamwomba kweli, basi Mungu anasikia na anaweza kuwaponya wote”.

Tumuombe Mungu atusaidie kutuepusha na mabalaa ya uvunjifu wa amani, tumlilie Mungu na Mungu wetu atajibu tuna imani hiyo. Ameongeza Mkuu wa Mkoa.

Sambamba na hayo RC Mtanda amewataka Viongozi hao kutojihusisha na siasa za ubaguzi anbazo zinapelekea kuharibu amani ya nchi ambayo ni tunu ya Taifa ikiwa imejengwa kwa misingi imara na ya muda mrefu.

Akizungumza mara baada ya kupokea wito huo Askofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Victoria Nyanza, Zephania Ntuza amesema maneno ya Mkuu wa Mkoa ni yamewafunua na kuwapa uelewa wa kina hivyo hawana budi kuyatekeleza kwa vitendo na watahakikisha wanatoa elimu hiyo ya amani kwa waumini wao.

Mpaka sasa Mkuu wa Mkoa amekutana na kufanya mazungumzo na makundi mbalimbali akilenga kuhamasisha amani na utulivu suala ambalo ameliita kama agenda ya muhimu.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.