RC MTANDA AWATAKA VIONGOZI WA DINI KUISAIDIA SERIKALI KUJENGA MAADILI MEMA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewataka Viongozi wa Dini kulitumia kundi kubwa la Waumini wanaowategemea kuwapelekea habari njema za kiroho ili wawe na utamaduni wa kuwa na matendo mema kwa kutumia imani zao.
Mkuu wa Mkoa ametoa rai hiyo mapema leo tarehe 19 Februari 2025 alipokuwa akitoa salamu katika Mkutano wa Sinodi Kuu (Baraza Kuu la Kanisa la Africa Inland Church Buzuruga Mwanza), ambapo amewataka Viongozi hao kuwakumbusha waumini wao wajibu wa kuishi maisha yenye maadili mema.
“Tukishirikiana vizuri kati ya Serikali na Viongozi wa Dini tutajenga Taifa lenye Watu Waadilifu na hivyo kupunguza kero nyingi zinazoikabili jamii katika
Nchi yetu”. Mhe. Mtanda.
Aidha, Mkuu wa Mkoa amesema uhusiano kati ya Serikali na Dini ni vitu ambavyo havitenganishiki, ni sura mbili za sarafu. Kwa sababu, binadamu ni
mwili na roho na kila kimoja hakina budi kuendelezwa kwani Serikali inashughulika na miili na akili huku Dini zinashughulika na roho.
“Naomba niwahakikishie AICT pamoja na ndugu zetu wanaounga mkono kazi mnazofanya kwamba serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwenu ili muweze kutimiza malengo yenu ya kulijenga Kanisa na kuwahudumia Watanzania”.
Kabla ya kuhitimisha hotuba yake Mkuu wa Mkoa amesisitiza kuhusu masula mbalimbali ikiwemo Umoja na mshikamano, kukuza Amani na Utulivu, kuongoza kwa hekima na uwajibikaji, huku akiwataka Viongozi hao wakizingatia maslahi ya jamii yote na kuwahudumia waumini kwa uaminifu na upendo.
Akizungumza Kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa, Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT Mhashamu Baba Askofu Musa Masanja Magwesela, amesema Sinodi Kuu iliyoketi leo inaundwa na Dayosisi 7 yani Dayosiis ya Geita, Mara ukerewe, shinyanga, Tabora, Pwani, na Tanga ambapo wachungaji wote wa Makanisa, Viongozi wa idara, wanawake na vijana wanakutana mara moja kwa miaka miwili ambapo kwa mara ya mwisho waliketi mwaka 2022.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.