Katika kuimarisha jitihada za kuboresha hali ya usafi wa mazingira na kuimarisha huduma za afya kwa wananchi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na halmashauri zake leo Julai 21, 2025 wameanza ziara ya siku 4 ya mafunzo Mkoani Iringa.
Kiongozi wa timu hiyo RMO Mwanza Dkt. Lebba amebainisha kuwa malengo kuwa ni kujifunza mbinu bora na mafanikio ya Mkoa wa Iringa katika kusimamia masuala ya afya na usafi wa mazingira, ili uzoefu huo uweze kutumika kuleta maboresho ndani ya Mkoa wa Mwanza.
Amesema, wakiwa mkoani humo washiriki watatembelea Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, ambapo wanatarajiwa kujifunza kwa vitendo juu ya mifumo ya usimamizi wa usafi wa mazingira, ushirikishwaji wa jamii, na mbinu za kuzuia magonjwa ya mlipuko kupitia mazingira safi.
Katika siku ya kwanza ya ziara hiyo Dkt. Lebba na timu yake wamefika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa na kujitambulisha kwa Mhe. Henry James Mkuu wa Mkoa huo na baadaye wamezungumza na Timu ya Menejimenti ya Afya Mkoa wa Iringa (RHMT).
Timu hiyo inajumuisha Afisa Afya wa Mkoa, Katibu wa Afya wa Mkoa, pamoja na Waganga Wakuu wa Halmashauri za Mkoa, pia inahusisha Maafisa Afya kutoka Halmashauri za Jiji la Mwanza, sengerema, misungwi na Ilemela.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.