Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Adam Malima leo Oktoba 18,2022 amezindua ujenzi wa kivuko kipya cha Rugezi-Kisorya, Ukerewe kinachojengwa na Kampuni ya Songoro Marine Transport.
Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) , Mhandisi Lazaro Kilahala amesema kivuko hicho kitagharimu Shilingi bilioni 5.5.
Kivuko hicho kikikamilika kitakuwa na uwezo wa kubeba abiria 800 na tani 170 za mizigo ikijumuisha magari madogo 22
Mhandisi Kilahala ameeleza kwamba mkataba wa ujenzi wa kivuko hicho ulisainiwa Juni 3, 2021 na ujenzi ulianza Desemba 15, 2021 na kinatarajiwa kukamilika Aprili 15, 2023.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Songoro Marine Transport Major Songoro ameahidi kwamba watajitahidi kuukamilisha kabla ya wakati ili kuwarahisishia wananchi usafiri.
"Tunaishukuru sana serikali kwa kuendelea kuthamini na kutupa miradi mbalimbali yenye manufaa kwa Taifa, tunaahidi tutaendelea kufanya kazi kwa weledi zaidi" amesema Songoro.
Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amesema serikali inaimani na TEMESA hivyo wafanye kazi ili kuhakikisha vivuko vyote vinavyojengwa na serikali vinakuwa na viwango vya kimataifa.
"TEMESA mtendeeni haki Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia vizuri miradi yote ya vivuko ndani ya ziwa Victoria na Tanganyika" amesema Mhe. Malima.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.