Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa kutumia fungu la asilimia 4 kutoka kwenye mapato ya ndani imetoa mkopo wa zaidi ya milioni 360 kwa vikundi vitano vya vijana na kuwawezesha kuanzisha shamba la ufugaji samaki kwa njia ya vizimba ndani ya ziwa victoria.
Akizindua shamba hilo katika mtaa wa Ihumilo kata ya Luchelele leo Agosti 25, 2025 Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Bw. Ismail Alli Ussi amewapongeza Viongozi wa Halmashauri na Wilaya hiyo kwa kuliwezesha Kundi hilo.
Kiongozi huyo amesema Halmashauri hiyo inatekeleza sera ya uchumi wa buluu kama dira ya kukwamua watu na uchumi kwani kwa kuinua mtaji yao na kuwawezesha kuwa matajiri wa siku za usoni na kwamba itawasaidia hata kuanzisha biashara zingine.
Aidha, ametoa wito kwa vikundi hivyo kuhakikisha wanarejesha mikopo hiyo ili makundi makundi mengine yaweze kukopeshwa pia na amewataka kuwa wazalendo na waadilifu na wenye kujiendeleza kielimu ili kufanya miradi yao kuwa endelevu.
Naye, Mwenyekiti wa umoja wa vikundi vya vizimba Ihumilo ndugu Ndongo Makina ameishukuru serikali kwa kuwawezesha mtaji huo huku akibainisha kuwa unakwenda kuinua maisha yao kwani wanafuata masharti na kanuni za biashara na uwekezaji wa miradi chini ya usimamizi ya wataalamu kutoka halmashauri hiyo.
Aidha, ameahidi kuendelea kufuata masharti ya ufugaji bora wa samaki katika kuhakikisha wanaendeleza masalia ya samaki pamoja na kutunza mazingira ya majini.
Katika wakati mwingine, Mwenge wa Uhuru umezindua Barabara ya kiwango cha zege katika mtaa wa Genge la hewa na kituo cha afya Mkolani, umekagua mradi wa nishati safi ya kupikia pamoja kuzindua kituo cha polisi katika mtaa wa Nyegezi ambacho kitakua msaada sana kwa abiria wa kituo cha mabasi cha eneo hilo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.