VIONGOZI WA CCK NA MAKINI TAIFA WAMPA KONGOLE RC MTANDA USIMAMIZI WA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA
Viongozi wa Vyama vya Makini na CCK Taifa wamempongeza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na Wasaidizi wake katika kuhakikisha uchaguzi Mkoani humo umefanyika kwa utulivu na amani.
Pongezi hizo zimetolewa na Viongozi hao mapema leo Novemba 28, 2024 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, na Mwenyekiti wa Makini Taifa Mhe. Coaster Kibonde na Mwenyekiti wa CCK Taifa Mhe. David Mwaijojele.
Akizungumza na Waandishi habari Mhe. Kibonde amesema Mkoa wa Mwanza ni Mkoa pekee ambao umeonesha dhahiri kuendana na zile R nne za Mhe. Rais Dkt. Samia kwa kusimamia na kutekeleza demokrasia kwa haki na usawa.
"Mimi kama Mwenyekiti wa Kitaifa nilipofika Mwanza tu niliuliza vipi kuna wagombea wowote walioenguliwa nilijibiwa hapana hakuna alienguliwa na ndivyo hali ilivyokuwa'. Mwenyekiti wa Chama cha Makini Taifa.
Naye Mwenyekiti wa CCK Taifa amesema kwa siku ya jana alifanikiwa kutembelea baadhi ya Vituo vya kupigia kura katika Mkoa wa Mwanza na kuwahoji baadhi ya wapiga kura kuhusu namna zoezi hilo lilivyokuwa likiendelea na kubaini kuwa hakukua na buguza ya aina yoyote, utulivu na amani vilitawala.
"Nawapongeza Mkoa wa Mwanza kwa utulivu na watu kushiriki kampeni mpaka jana uchaguzi kwa amani na utulivu licha ya uwepo wa mvua kubwa hata kuengua engua hatujaskia kabisa hivyo nawapongezeni sana na ninampa RC Mtanda Big Up". Mhe. Mwaijojele.
Kuhusu kushinda au kushindwa Viongozi hao wamesema wataendelea kuwapongeza na kuwaunga mkono wale wote watakaoshinda kwa kuwa sasa uchaguzi umeisha na zoezi lililobaki ni kuungana kama Taifa na kujadili kuhusu maendeleo.
Aidha Viongozi hao wameishukuru Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kusimamia vyema uchaguzi kuanzia zoezi la uchukuaji fomu mpaka upigaji kura uliofanyika hapo jana ambapo zoezi linaloendelea kwa sasa ni utangazaji wa matokeo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.