Naibu Katibu Mkuu OW- TAMISEMI Bw. Sospeter Mtwale ametoa rai kwa wakuu wa Vitengo katika Ofisi za wakuu wa mikoa kusimamia kwa dhati miradi ya serikali ili ikamilike kwa wakati na kwa kuzingatia viwango kulingana na thamani halisi ya fedha zilizowekwa.

Bwana Mtwale ametoa wito huo mapema leo jijini Dodoma alipokua akifungua mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Viyengo vya Huduma ya Sheria, TEHAMA, Ufuatiliaji na Tathmini pamoja na Mawasiliano Serikalini kutoka katika mikoa ya Tanzania bara.

Aidha, amewataka kusimamia kwa dhati utatuzi wa migogoro kwa kuwasikiliza wananchi na kuwaondolea kero zao kwa wakati ili wasitumie muda mwingi kwenye mashauri badala yake wajikite kwenye kujitafutia kipato kupitia shughuli za kiuchumi.

Ameongeza kuwa kiongozi mzuri ni yule anayeweza kujenga timu ya pamoja na kusimamia utendaji kazi wa watumishi walio chini yake, hivyo anayo imani ya watendaji hao kubadirika endapo mtabaini kuwa kuna sehemu walikua wanakosea.
Naye, Mkurugenzi Msaidizi Tawala za Mikoa OWM-TAMISEMI Ibrahim Minja amesema Mafunzo hayo yameandaliwa ili kuwajengea uwezo viongozi hao katika vitengo wanavyovisimamia pamoja na kuwakumbusha wajibu wao katika kuzishauri halmashauri pamoja na kumsaidia Katibu Tawala wa Mkoa.

“Taasisi ya Uongozi inawajenga viongozi katika kusimamia taaisi kimifumo, kanuni, fedha pamoja na kusimamia watu na kumjenga kiongozi aonekane ndiye bila mashaka”, amesema Bw. Kadari Singo, Afisa Mtendaji Mkuu Taasisi ya Uongozi.

Kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza mafunzo hayo ya siku nne yamehudhuriwa na wataalamu kutoka kwenye vitengo vinne vya Mawasiliano Serikalini, Ufuatiliaji na Tathmini, TEHAMA huku wakiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha huduma za Sheria Bi. Nuru Mwambuli.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.