*BARABARA MPYA YA LAMI KUCHOCHEA MAENDELEO KATA YA KIRUMBA-ILEMELA*
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Ndugu Abdalla Shaib Kaim leo Julai 14, 2023 amezindua barabara ya Lami Nzito na Zege Magomeni- Kirumba- Kabuhoro- Ziwani wilayani Ilemela yenye urefu wa KM 0.9 iliyojengwa na Mkandarasi Nyanza Road Works.
Akizindua mradi huo ndugu Kaim ameupongeza Uongozi wa Manispaa ya Ilemelaa kwa usimamizi madhubuti wa kazi iliyogharimu zaidi ya Milioni 998 hali iliyopelekea ubora unaotakiwa na viwango thabiti vilivyotarajiwa.
"Mradi upo vizuri na umezingatia viwango" amesisitiza kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru wakati wa uzinduzi baada ya kukagua barabara na kuridhika na ubora na viwango kutokana na thamani ya fedha iliyotumika.
Naye Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angelina Mabula amemshukuru Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Fedha za Mradi huo kwani barabara hiyo imeondoka kero kubwa ya usafiri kwa wananchi wa kata ya Kirumba hasa wa kwenye makazi ya miinuko.
Katika wakati mwingine, Kiongozi wa mbio za Mwenge amewapongeza Ilemela kwa kutekeleza vema Ujenzi wa wodi ya wajawazito kwa zaidi ya Milioni 199 kwenye Kituo cha Afya Buzuruga ambapo shughuli ya Uzinduzi wa jengo hilo ilienda sambamba na ugawaji wa vyandarua kwa akinamama katika hatua za kuwakinga dhidi ya ugonjwa wa Malaria.
Kabla ya kufika kwenye Mradi wa kugawa vifaa vya kufanyia usafi na zoezi la usafi kiloleli, Mwenge wa uhuru ulifika kwenye Shule ya wasichana ya Bwiru ambapo viongozi hao na wa wilaya walipanda miti ya matunda 3000 katika kuhamasisha uhifadhi wa mazingira na lishe bora na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru akahimiza utunzwaji.
Vilevile, Mwenge wa uhuru ulimulika mradi wa Vijana wa ufugaji kuku Nyasaka na ukapongeza Halmashauri kwa kuwapatia mkopo wa Milioni 15 kikundi hicho pamoja na kitoa elimu ya Ufugaji na wakatoa wito kwa Halmashauri kuwakopesha zaidi wakimaliza marejesho na mwisho ukaweka Jiwe la msingi kwenye Ujenzi wa Bweni la wanafunzi Buswelu shule ya msingi.
Kaulimbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 inasema "Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa viumbe hai kwa Uchumi wa Taifa."
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.