Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Adam Malima amelishauri Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kuangalia upya adhabu zake kwa wanaokiua Sheria kutokana na zilizopo kuonesha kupitwa na wakati.
Akizungumza na ujumbe wa Baraza hilo ulioongozwa na Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi Ramadhan Ng'anzi, Mhe. Malima amesema kumekuwa na hali ya kutozingatia sheria zilizopo kutokana na watumiaji kuona wepesi wa adhabu husika.
"Unakuta mtu anatumia kilevi huku gari lake limebeba abiria na inapotokea amesabanisha ajali na kuuwa watu anaishia kuonekana uraiani na kulipa adhabu ndogo, hii siyo sawa". Amesisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.
Mhe.Malima amebainisha kuwa amepania kuuweka Mkoa wa Mwanza kama mfano wa kutokuwa na ajali kutokana na sheria zote za barabarani kuziwekea mkakati wa kuheshiwa na watumiaji wake.
"Tutaanza na kuweka ujumbe mahususi kwenye mabango yatayowekwa kwenye barabara kuu zote zinazoingia Mkoani Mwanza zinazowataka watumiaji kuzingatia sheria zote husika".Mhe Malima
Amesema, amepoke kwa dhati maamuzi ya kuufanya Mkoa wa Mwanza kuwa mwenyeji wa Sherehe za Kitaifa za Usalama Barabarani ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt Hussein Mwinyi.
Kwa upande wake Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kamishna Msaidizi mwandamizi Ramadhan Ng'anzi amesema mchakato wa marekebisho ya adhabu kwa wanaokwenda kinyume upo mbioni kufanyiwa kazi.
Sherehe za Kitaifa za Usalama Barabarani zitafanyika kuanzia tarehe 13 hadi 17 Machi mwaka huu Mkoani Mwanza zikitanguliwa na wiki ya Usalama Barabarani ambapo elimu mbalimbali zitatolewa kuhusiana vyombo vya moto vitumikavyo eneo hilo na haki ya mwenda kwa miguuu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.