BULABO IWE TAASISI ITAKAYOJISIMAMIA, YENYE WIGO WA KITAIFA NA KIMATAIFA: RC MTANDA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Said Mtanda leo ameendelea kukutana na makundi mbalimbali akianza mkutano wake na Machifu amesema mpango uliopo ni kuhakikisha Tamasha la utamaduni wa kabila la Wasukuma la Bulabo linakuwa ni Taasisi imara itakayojisimamia na kuwa na wigo wa mpana nchini na nje ya Tanzania.
Muendelezo wa mkutano huo unaofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mhe.Mtanda amebainisha kutokana na umuhimu wa tamasha hilo mwaka huu litakuwa na sura ya kikanda kwa kuunganisha mikoa ya Kanda ya ziwa na Tabora.
"Tayari tumefanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Prof. Adilaus Kilangi ametoa ushauri huo pia tamasha la mwaka huu tumewaalika wenzetu kutoka huko Amerika ya Kusini pia na sisi tutakwenda huko kubadilishana uzoefu na kujifunza zaidi," Mkuu wa Mkoa.
Amesema tamasha hilo linapaswa kwenda pamoja na makongamano yatakayowahusisha wataalamu wa masuala ya utamaduni, vyakula vya asili na mavazi ili kila wakati wa maadhimisho hayo kuwepo na mabadiliko.
"Nawakikishia Machifu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imelipokea jambo hili na itatoka ushirikiano wa dhati kuhakikisha Bulabo ya mwaka huu inakuwa bora zaidi niwaombe sana Machifu tuendelee kuisaidia Jamii ili kujivunia mila na desturi zetu,"Mkuu wa Mkoa.
"Sherehe za mwaka huu zitafanyika Juni 22 badala ya mwanzoni mwa mwezi huo,hii ni kutokana na kuwashirikisha wenzetu kutoka Brazil ambao tarehe za mwanzoni hawataweza kufika,"Jackson Kadutu,Katibu wa Bulabo.
Katika mkutano uliofuata na Baraza la Wazee wa Mkoa wa Mwanza,Mkuu huyo wa Mkoa amesema Ofisi yake itaendelea kupokea ushauri wa masuala mbalimbali ya maendeleo na kuwakumbusha mamlaka husika kutoa kipaumbele kwa wazee katika suala la kupatiwa matibabu bure.
"Umoja huu una wanachama hai 38 na lengo letu ni kuishauri Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kufuatilia shughuli mbalimbali ikiwemo miradi inayoletwa na Serikali mkoani hapa,"Charles Masalakulangwa,Mwenyekiti Baraza la Wazee Mwanza.
Mkutano wake wa mwisho na wadau wa Sekta ya Utalii,Mkuu huyo wa Mkoa amepokea maoni namna ya kuiboresha sekta hiyo inayochangia 17% ya pato la Taifa na kutaka mikakati zaidi ifanyike kutokana na Serikali kuimarisha miundombinu ukiwemo upanuzi wa uwanja wa ndege.
"Niwape muda zaidi wa kukaa na kuona namna ya kuwashirikisha wadau wengine zaidi kabla ya sijaitisha kikao kikubwa zaidi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.