CCM MKOA YAKAGUA MIRADI YA SHS BILIONI 7 KWIMBA
Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba leo Mei 24, 2024 imekaguliwa miradi yake 6 ya maendeleo yenye gharama ya shs bilioni 7 na kamati ya Siasa ya Mkoa wa Mwanza na kupewa maagizo mbalimbali.
Kamati hiyo ukiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoani humo Mhe.Michael Lushinge ameiagiza Halmashauri ya Kwimba kuhakikisha vituo vyote vya afya vinatoa huduma kwa kufuata mfumo wa kidijiti ambao ni bora na unadhibiti mapato.
"Hongereni kwa miradi hii ya maendeleo lakini hapa kituo cha afya Budushi naona bado wanatumia mfumo wa kizamani wa kupokea pesa mbichi hii siyo sawa badilikeni haraka",Lushinge.
Amesema amefurahishwa kusikia awali wananchi wametumia nguvu zao za gharama ya shs milioni 16 kujenga kituo hicho,hali ambayo inaonesha wanajali maendeleo yao kabla ya Halmashauri kutumia mapato ya ndani kwa kutoa zaidi ya shs milioni 321 na TASAF kutoa shs milioni 356 kukamilisha kituo hicho
Kamati hiyo iliyoanza kukagua mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya maabara za sayansi na bweni shule ya Sekondari Nyamilama yenye thamani ya zaidi ya shs milioni 200 na kuwataka walimu wazidishe juhudi ya ufaulu kutokana na Serikali kuzidi kuboresha miundombinu shuleni.
Ikiwa kwenye ukaguzi wa Hospitali ya wilaya ambayo tayari imeanza kutoa huduma na kugharamiwa na Serikali Kuu zaidi ya shs bilioni 3
"Mhe.Mwenyekiti Hospitali yetu ya wilaya kama uionavyo imeanza kutoa huduma na tunaendelea baadhi ya kuboresha miundombinu na tumepokea vifaa tiba vya kisasa vinavyo tufanya kutoa huduma bora,"Happiness Msanga,Mkurugenzi H/Kwimba
Katika ukaguzi wa ujenzi wa Jengo la Utawala la Halmashauri hiyo kwa gharama ya zaidi ya shs bilioni 3 kwa njia ya force account,Kamati imepongeza kwa kumtoa mkandarasi wa awali kwa kuonesha ubabaishaji na kuishauri kutumia vizuri fedha katika hatua ya umaliziaji ambayo ina vitu vingi vya gharama.
Ikihitimisha ziara hiyo kwenye shule mpya ya Sekondari ya Bumyengeja iliyojengwa kwa gharama ya zaidi ya shs milioni 500,Kamati hiyo imeipongeza Halmashauri kwa kuwapunguzia wanafunzi umbali mrefu wa kutembea na pia udhibiti wa utoro.
Katika taarifa yake fupi wakati wa majumuisho Mkuu wa Wilaya ya Kwimba,Mhe.Ng'wilabuzu Lidigija aliyezungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa ameishukuru Kamati hiyo kwa ukaguzi na kutoa maagizo sehemu zenye kasoro na kuahidi kuyatekeleza.
"Mhe Mwenyekiti yale yote uliyoyatolea maagizo kuanzia kwenye kituo cha afya,shule,hospitali na jengo la Utawala tumeyapokea na tunayafanyia kazi ili lengo letu litimie la kutoa huduma bora kwa wananchi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.