Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Adam Malima amekitaka Chama cha Ushirika Nyanza kupiga hatua kwa kuwa na nguvu ya kiuchumi kwa kumiliki Benki,Viwanda na Mashamba.
Akizungumza leo kwenye Mkutano mkuu wa 31 wa Chama hicho uliofanyika Chuo cha ualimu Butiama, Mhe.Malima amewataka wajumbe wa Mkutano huo kuwa chachu ya maendeleo ya Chama hicho kwa kuwa na sura mpya ya kiuchumi kila mwaka.
"Kupiga hatua si Jambo lele mama ni lazima kwanza mjenge nidhamu ya uwajibikaji na bila kuoneana aibu kuwajibishana mkifanya hayo matunda ya maendeleo mtayaona". Amesisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.
Amewahakikishia fedha yao Shs Bilioni 1.4 ambayo imetolewa maelekezo na Serikali ipo salama na kuwataka kuondokana na fikra za kuzichukua na kuzifanyia matumizi ndani ya Ushirika huo badala yake fedha hizo ziwe mtaji wa kukopesheka kwenye Taasisi za mabenki.
Amemuagiza Mrajisi wa Ushirika Mkoa Lucas Kiondele kuunda timu hiyo itakayomletea taarifa ya mwelekeo wa Ushirika huo na mkakati wao ujao wa kiuchumi.
"Chama cha Ushirika Nyanza kwa kuwashirikisha wanachoma wake kina utaumia vizuri Uchumi wa bluu kwa kufanya Uvuvi wa kisasa wa kutumia Vizimba ambao umekuwa na tija kwa kutumia gharama ndogo na kupata faida kubwa"Emil Kasagara,Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.