DC UKEREWE AWATAKA WAJASIRIAMALI KULITUMIA JUKWAA LA NANENANE KUJA NA MAGEUZI CHANYA YA KILIMO
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mh.Chtustopher Ngubiagai amefurahishwa na mwamko wa wajasiriamali waliojitokeza kwenye maonesho ya Nanenane Mwanza na kuwataka kuyatumia ili kuzidi kuelimika katika shughuli zao mbalimbali za kiuchumi.
Mkuu huyo wa Wilaya akiambatana leo Agosti 2,2024 na mkuu wa Idara ya Uchumi na Uzalishaji kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Bw.Emil Kasagara amesema amejionea Taasisi mbalimbali zilivyojipanga kuwaelimisha wajasiliamali na wananchi kwa ujumla namna ya kufanya shughuli zao kitaalamu.
"Nimepitia kwenye baadhi ya bustani za mazao mbalimbali nimefurahishwa sana namna ya ustawishaji wa mazao kama mahindi na miti ya mitunda inavyolimwa kitaalamu kuanzia upatikanaji wa mbegu bora",amesema Mkuu huyo wa Wilaya mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea mabanda ya Nanenane.
Mkuu huyo wa Wilaya amebainisha hivi sasa pesa ya uhakika ipo shambani ukiamua kuwa mkuiima wa mazao au mfugaji kwani kila kitu sasa kinafanyika kwa utaalamu wenye tija na siyo kama zamani kufanya shughuli kwa mazoea,"Mhe. Ngubiagai
Amewapongeza waandaaji wa maonesho hayo ambayo ni mikoa mitatu kutoka Kanda ya ziwa magharibi Mwanza,Geita na Kagera kwa kuzidi kuinua shughuli za kiuchumi kwa wananchi kwani ndiyo nia ya Rais Samia ya kuona wananchi wanazidi kusonga mbele katika maendeleo yao.
Naye Bw.Kasagara amebainisha maonesho ya mwaka huu wameyapa hamasa ya kutosha kwa kuanza kuyatangaza kuanzia mwanzoni mwa Julai ili wananchi wapate uelewa wa kutosha na kujitoleza kwa wingi.
"Kwenye maonesho haya kuna kila aina ya huduma zinazotolewa na Taasisi mbalimbali zikiwemo za kifedha kwa wale wafanyabiashara kuanzia wa chini,kati hadi wa juu watapata fursa za kuelimishwa namna ya kuendesha shughuli zao kitaalamu na upatikanaji wa mikopo kwa unafuu,"Kasagara
Maonesho hayo yaliyobeba kauli mbiu isemayo Chagua viongozi bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo endelevu ya Mifugo,Kilimo na Uvuvi, yatafunguliwa rasmi Agosti 3,2024 na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Martin Shigella.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.