DKT. KIDA ARIDHISHWA NA UWEKEZAJI UNAOFANYWA MWANZA
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Dkt. Tausi Kida amepongeza jitihada zilizofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda katika uwekezaji na kuufanya Mkoa huo kuwa namba mbili nchini kwa uwekezaji.
Dkt. Kida ameyasema hayo leo Julai 19, 2024 wakati alipomtembelea Ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa lengo la kujitambulisha akiwa katika maandalizi ya kongamano la wadau na wananchi wa kanda ya ziwa kwa ajili ya ukusanyaji wa maoni kuhusu maandalizi ya dira ya Taifa ya maendeleo ya mwaka 2050 linalotarajiwa kufanyika hapo kesho katika ukumbi wa Rock City Mall.
"Lengo la kongamano hili ni kuchukua maoni ya wananchi wa kanda ya ziwa, wao wanadhani dira yetu iwe na nini na nini ndio maana tupo hapa tunataka kusikia na kuyachukua maoni hayo kwa ajili ya utekelaji". Dkt. Kida.
Ameongeza kuwa pamoja na kuwekeza kwa zaidi ya miradi 180 mkoani humo, eneo la ujenzi ndio limeongoza zaidi likifuatiwa na reli ya mwenso kasi (SGR) kwani limeiweka Mwanza kwenye ramani kwa kutoa fursa ya kuwekeza kwenye kongani pembezoni mwa Reli.
Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameishukuru Wizara ya Mipango na Uwekezaji kwa kuamua kulifanyia kongamano hilo Mwanza kwa kuwa ndio kitovu cha uchumi na uwekezaji kwa Mikoa ya Kanda ya Ziwa.
"Hapa Mwanza ndio kitovu cha uchumi wa Mikoa ya Kanda Ziwa, maandalizi ni mazuri na tumejipanga vyema, ninawashukuru hamkuona sababu ya kukusanya na kuzichukua barua tu bali mmeamua kuwafuata wananchi wenyewe kwa ajilli ya kuwasikiliza na wapongezeni na karibu sana". Amesema Mhe. Mtanda.
Aidha, Mhe. Mtanda amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia imefanya uwekezani mkubwa katika Mkoa wa Mwanza ikiwemo upanuzi wa bandari, ujenzi wa kituo cha uokozi ndani yq ziwa, ujenzi wa daraja la kigongo - Busisi, ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR, vizimba vya kisasa kwa wavuvi pamoja na ujenzi wa meli kubwa ya kisasa ya Mv. Mwanza Hapa Kazi Tu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.