ENDESHENI KISASA NA KWA UFANISI STENDI YA MABASI YA NYAMHONGOLO-RC MAKALLA
*Amshukuru Rais Samia Suluhu kwa kutoa Bilioni 24 kujenga Stendi ya kisasa
*Ashauri uongozi wa Halmashauri ya Ilemela kwenda kujifunza zaidi namna ya uendeshaji kwenye Stendi za Magufuli na Msamvu
*Aagiza TABOA,LATRA, RTO na uongozi wa Halmashauri ya Ilemela kukutana kuboresha huduma ya usafirishaji
Halmashauri ya Ilemela imepongezwa kwa kuwa na Stendi nzuri ya Mabasi ya abiria na ya mfano na kushauriwa kwenda kujifunza zaidi kwenye Stendi za Magufuli na Msamvu namna bora ya uendeshaji ili watoe huduma ya kiwango cha juu kuendana na hadhi ya Stendi hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.CPA.Amos Makalla ametoa kauli hiyo leo mara baada ya kufanya ziara fupi ya kukagua uendeshaji wa Stendi hiyo iliyoanza kutoa huduma rasmi Agosti 16,2022,amesema majengo ya Hosteli sasa yabadilishwe hadhi na kuwa Hotel au Lodge na kutafutiwa mzabuni mwenye uzoefu mzuri.
"Nimeifanya kazi Mikoa kadhaa lakini Stendi hii ni ya kiwango cha juu nimeona ukubwa wake na namna ilivyopangiliwa ikiwemo Karakana ya kisasa ya magari,na majengo haya ya kulala mnayoita Hostel hapa naiona kasoro kidogo haipaswi kuitwa hivyo",CPA Makalla
Mhe.Makalla amebainisha baada ya kulikagua jengo hilo la kulala lina hadhi ya kuitwa Hotel au Lodge na jitihada za haraka zifanywe za kumpata mzabuni atakayeindesha Hotel hiyo na Halmashauri kujihakikishia mapato.
"Serikali huwa haifanyi biashara hapa mkisema muiendeshi wenyewe haitawezekana,tumieni utaratibu mzuri na nina imani mtampata mtu sahihi wa kufanya shughuli hii",amesisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.
Kuhusu utoaji wa huduma bora kwa wananchi Mhe.Makalla ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Ilemela,LATRA,TABOA na RTO kukutana ili kukubaliana namna bora ya utoaji wa huduma za mabasi hasa yaendayo Mikoa ya kati ambayo safari zake huanzia Stendi ya Nyegezi.
"Baada ya kikao hiki naomba nikutane mchana huu Ofisini kwangu na wakurugenzi wa Halmashauri zote mbili Nyamagana na Ilemela na wadau wa usafirishaji ili tupate mwafaka mzuri wa kuwaboreshea huduma wananchi",CPA Makalla.
"Mhe Mkuu wa Mkoa tumefarijika na hii ziara yako ambayo imebeba mambo mengi ya kuwahudumia wananchi,tunakuahidi maagizo yote tutayafanyia kazi",Mhe.Hassan Masalla,Mkuu wa Wilaya ya Ilemela.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe.Dkt.Anjelina Mabula amesema miradi mingi ya kimkakati iliyopo Mkoani Mwanza ina kila sababu ya kusimamiwa vyema ili iwe na tija kwa wananchi.
"Mhe Mkuu wa Mkoa naomba niombe radhi kwa changamoto mbalimbali zilizotolewa na wahusika na usafirishaji wa abiria kwenye Stendi hii ya Nyamhongolo,lengo letu ni tuwe mfano wa utoaji wa huduma bora siku zote",Kiomoni Kibamba,Mkurugenzi Halmashauri Ilemela.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.