Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe Mhandisi Robert Gabriel amewakaribisha wananchi wa Mkoa huo kwenye kuitambulisha rasmi kwa kuiangalia filamu ya Royal Tour hafla itakayofanyika kwenye Viwanja vya Rock Ciy siku ya tarehe 18 Juni 2022.
Akizungumza kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari mapema leo, Mkuu wa Mkoa amesema Utambulisho huo rasmi utatanguliwa na shughuli mbalimbali ambapo Juni 16, 2022 watu zaidi ya mia moja watatembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na tarehe 17,06, 2022 kutakua na ziara ya kutembelea vivutio vya utalii vya Jiji la Mwanza na Safari za Ziwani.
"Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imeandaa tukio hili mahsusi kwa ajili ya kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hasaan kuitambulisha Sekta ya Utalii nchini ya kuvitangaza Vivutio vya Utalii na utamaduni wetu" amefafanua Mkuu wa Mkoa.
Aidha, Mhe. Mkuu wa Mkoa amebainisha kuwa Filamu ya Royal Tour mpaka sasa imetazamwa na watu wa Mataifa mbalimbali Duniani hivyo kutakua na ongezeko la idadi ya Watalii wanaotembelea nchi yetu na kuongeza pato la nchi sambamba na uwekezaji kwenye sekta mbalimbali.
"Kupitia kuitambulisha rasmi filamu ya Royal Tour Mkoani Mwanza watapata fursa ya kutembelea vivutio vya Utalii kama Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saa nane, Jiwe la Bismark, Gunzert House na malumbusho ya Kabila la wasukuma ya Bujora."
Mhe Mkuu wa Mkoa amefafanua kuwa Filamu ya Royal Tour iliyofanywa na Mhe Rais Samia Suluhu Hasaan imeonesha vivutio vya utalii nchini kama vile Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Ngorongoro, Fukwe za Zanzibar, utalii wa utamaduni pamoja na Madini ya Tanzanite.
"Utambulisho rasmi wa Filamu ya Royal Tour Mkoani Mwanza utautambulisha Mkoa kama lango kuu la kuingilia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ukizingatia kwamba inawachukua Watalii takribani saa mbili na nusu kufika kwenye Hifadhi hiyo wakitokea Mwanza," amesema.
Vilevile, Mkuu wa Mkoa amemshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi za kuboresha Miradi mikubwa itakayokuza na kuendeleza Utalii Mkoani Mwanza kupitia Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya Mwendo Kasi, Ujenzi wa Daraja la Busisi na ukarabati mkubwa wa Uwanja wa ndege wa Mwanza hususani kwenye ujenzi wa jengo la abiria.
Utambilisho wa Filamu hiyo yenye dakika 56 Mkoani Mwanza utatanguliwa na burudani kutoka vikundi vya ngoma za asili na wasanii mbalimbali kuanzia saa 9 Alasiri hadi saa 1 jioni na utakuwa na washiriki takribani 1000.
_Mwisho_
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.