FURSA ZA KIUCHUMI ZACHOMOZA KWENYE MDAHALO WA KITAIFA,MWANZA
Mdahalo wa Kitaifa kuhusu ubia kati ya sekta ya umma na binafsi umefanyika Jijini Mwanza, ukilenga kuchochea ushirikiano endelevu kwa maendeleo ya kiuchumi kwa ujumla.
Akizungumza katika mdahalo huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi, Chagu Ng'h'oma, Katibu Tawala msaidizi sehemu ya Miundombinu amesema Mkoa wa Mwanza ni kitovu muhimu cha uchumi wa Kanda ya Ziwa kutokana na nafasi yake ya kipekee kijiografia na uwepo wa Rasilimali hiyo
"Mwanza ni lango kuu la biashara ndani na nje ya nchi kupitia Ziwa Victoria. tunawakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza katika uchumi wa bluu hasa uvuvi, usafirishaji majini, na utalii wa ziwani pamoja na sekta ya ufugaji wa kisasa wa samaki kwa njia ya vizimba,"
Ameongeza kuwa Serikali ya Mkoa wa Mwanza imeweka mazingira rafiki kwa wawekezaji, ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara, bandari, na maeneo ya viwanda, ili kuhakikisha miradi ya ubia kati ya sekta ya umma na binafsi inatekelezwa kwa ufanisi.
Akizindua mdahalo unaohusisha makundi mbalimbali ya jamii ikiwemo sekta binafsi na wanahabari kuhusu dira ya Taifa ya maendeleo ya mwaka 2050 jijini Mwanza, Naibu waziri wa nchi ofisi ya Rais mipango na uwekezaji Stanslaus Nyongo amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ili kila mtanzania kutumia fusra zilizopo.
Kwa upande wake Mkurungenzi Mtendaji wa kituo cha ubia katia ya sekta ya umma na binafsi PPPC David Kafulila amesema kutokana na ufanisi wa ushirikiano kati ya sekta hizo mbili Serikali inalenga kuongeza uwekezaji katika miradi mbalimbali.
Mdahalo huo umetajwa kuwa jukwaa muhimu la kuibua changamoto, mafanikio na mikakati ya kuendeleza miradi ya maendeleo kupitia ubia huo, huku wito ukitolewa kwa sekta binafsi kuchangamkia fursa zilizopo ndani ya mkoa huo na Tanzania kwa ujumla.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.