Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdullah Ulega amefanya ziara Wilayani Misungwi katika kituo cha Uzalishaji Mifugo Mabuki kwa lengo la kukabidhi Ng'ombe dume 36 aina ya (Boran Heifer) kwa muda Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mhe. Senyi Ngaga kwa ajili yakuongeza tija ya ufugaji kwenye Halmashauri ya Buchosa.
Kabla ya makabidhiano hayo Mhe.Ulega amezungumzia namna Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alivyoamua kuongeza thamani ya ufugaji kupiti program ya
"Samia ufugaji wenye tija" ametoa jumla ya Shilingi Bilioni 3.5 kwa Nchi nzima ili zikaongeze tija, katika fedha hizo Shilingi Milioni 878.4 zimetumika kununua ng'ombe Dume 366 huku 36 wakiletwa Buchosa.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mhe. Senyi Ngaga ametoa shukrani kwa kukabidhiwa ng'ombe hao kwa ajili ya Halmashauri ya Buchosa. "Hii ni fedha na tungetamani pia haya tunayosema tuyaone kwa vitendo na tija inakuwepo".Mkuu wa Wilaya
"Mkoa wa Mwanza unajumla ya ng'ombe 1,175,000 kimsingi Mifugo hiyo inatoa mchango mkubwa kuinua uchumi kwa watu wa Mkoa huu na kwa Serikali kwa ujumla"Emily Kasagara Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji
Aidha Mhe Ulega amesema haya yote yanafanywa kwa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020 ambayo imewaelekeza kuhakikisha Serikali inakuwa na mikakati mbalimbali inayopelekea kufanya shughuli za watanzania kujiongezea kipato na kuongeza mchango wa sekta ya Mifugo na Uvuvi uwe mkubwa katika pato lake.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.