Hongereni kwa huduma ya Maji Vijijini, Ongezeni bidii mfikie malengo ya asilimia 85: RAS Balandya
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Balandya Elikana amewapongeza Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kwa uboreshaji wa huduma ya Maji na amewataka kuongeza bidii ili kufikia lengo la asilimia 85 ifikapo mwakani.
Akizungumza leo kwenye kikao kazi cha watumishi wa Ruwasa kwenye ukumbi wa Mikutano Rocky City Mall, Balandya amesema kumekuwa na ongezeko zuri la upatikanaji wa rasilimali niyo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2019 ikianza na 49% na sasa imefika 70%.
"Vikao kama hivi mnavyofanya kila mwaka vya kujitathmini utendaji wenu wa kazi ni muhimu kwani vitaongeza uboreshaji wa kazi zenu za kuwahudumia wananchi," amesisitiza Mtendaji huyo wa Mkoa wakati akizungumza na watumishi hao.
Amesema Rais Samia amedhamiria kuwaondeoea kero ya maji wananchi kwa kutoa fedha nyingi za miradi hiyo, hivyo ni wajibu wa watumishi hao kuhakikisha wanaisimamia kwa weledi miradi hiyo na inakamilika kwa wakati
Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Godfrey Sanga amebainisha kuwa kupitia kikao kazi hicho wanapata fursa ya kujadiliana changamoto mbalimbali na kuzipatia ufumbuzi lengo likiwa ni kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi vijijini.
"Tuna miradi 75 ya maji Vijijini inayoendelea kutekelezwa, mkakati wetu ni kuhakikisha tunaikamilisha kwa wakati ili kuwaletea maendeleo wananchi," Mhandisi Sanga.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.