Leo jumatatu Juni 13, 2022, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe Mhandisi Robert Gabriel amekagua huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sekou Toure baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Mradi wa jengo la Mama na Mtoto lililogharimu Shilingi Bilioni 9.8.
Akizungumza na wagonjwa na wauguzi, Mhe Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa wananchi kupata huduma bora na za kibingwa kwenye Hospitali hiyo na zingine zote kwani kuna uboreshaji wa huduma kwa kiwango kikubwa kwenye hospitali zote Mkoani humo.
"Mhe Rais Samia Suluhu Hassan amevunja rekodi yake mwenyewe, ameboresha huduma za Afya kwa kiwango kikubwa na anahakikisha kila mtanzania anapata huduma bora kuanzia huduma za Msingi hadi za kibingwa kwakweli tunampongeza sana." Mhe Robert Gabriel.
"Mkuu wa Mkoa, ndani ya Mkoa wako kuna Miradi Mikubwa mingi ya Afya inaendelea kwa kasi kubwa karibia kila kona kama Bugando na Nansio Wilayani Uk hierewe yenye takribani zaidi ya Bilioni 40." Amesema Mganga Mkuu wa Mkoa, Thomas Rutachunzibwa.
Akitoa taarifa, Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dktr Bahati Msaki amesema hospitali hiyo inahudumia wagonjwa wa nje kati ya 450 hadi 500 kwa siku na 80-100 wanaolazwa na mama 25-30 wanajifungua kawaida huku 3-10 wakijifungua kwa upasuaji kwa siku.
"Kupitia uboreshaji wa huduma, tumefanikiwa kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kutoka vifo 18-2017 hadi vifo 8-2021 na kutoka januari 2021 hadi disemba 2021 tumepokea akina mama waliokua kwenye hali mbaya 191 ambao walihudumiwa na kupona " Amesema Mganga Mfawidhi.
Aidha, amefafanua kuwa jengo hilo la ghorofa tano lina uwezo wa kubeba vitanda 261 ambapo hadi kukamilika kwake litagharimu Bilioni 10.1 na kwamba hadi sasa limefikia asilimia 97 za Ujenzi huku fedha iliyopokelewa ikiwa ni Tshs Bilioni 9.8 .
"Mhe Mkuu wa Mkoa, sisi kama Chama Cha Mapinduzi tunafarijika sana kwa jinsi Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anavyoleta fedha kutekeleza miradi mbalimbali nchini" Mhe Godfrey Kavenda Katibu CCM Wilaya ya Nyamagana.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.