Jamii imetakiwa kutonyamazia na kuficha watu wanaofanya ukatili kwa watu wenye ualibino ukiwemo ukatwaji viungo.
Akiongea mara baada ya kuzindua kambi (summer camp) kwa ajili ya wanafunzi wenye ualbino kujifunza vitu mbalimbali, michezo na kujuana, Muasisi na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Under The Same Sun(Utss) Peter Ash alisema takwimu ambazo wanazo za mauaji na mashambulizi kwa watu wenye ualibino ni chache kulinganisha na uhalisia wa matukio yanayotokea kwenye jamii.
Alisema kwa data walizokusanya mwaka 2008 kulikuwa na mauaji na shambulizi 40, mwaka 2018 mashambulizi nane na mwaka 2019 mwanzoni yalitokea mashambulizi mawili.
"Mara nyingi matukio hayo hayatolewi taarifa kwa sababu watu wa familia hizo uhusika, japo yamepungua hatuwezi kufurahia hadi idadi itakapofika sifuri"alisema Ash
Akizungumzia uamuzi wa kuweka kambi ya wanafunzi kwenye chuo cha ualimu Butimba, Mchungaji kutoka Canada, Pastor Brad Samour alisema lengo la kambi hiyo ni kuwapatia fursa wanafunzi ya kujua vipaji vyao.
"Tunawapatia nafasi ya kufanya sanaa, michezo, kujifunza kwa vitenda na wengi wana vipaji" alisema
Wanafunzi walioudhuria kambini Semeni Eliakimu na Benedictor Felcian waliitaka jamii kuachana na imani kuwa watu wenye ualbino hawawezi kifanya vitu vya msingi kwani wanao uwezi kama wengine.
"Jamii yetu tunakuwa ni watu tunaodharaulika sana, kuwa hatuwezi kitu chochote lakini nakanusha. Sisi ni watu kama watu wengine na tunaweza kutimiza malengo na ndoto zetu",alisema Eliakimu
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.