Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene, amelitaka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini, kuwachukulia hatua wanafunzi wanaohujumu miundombinu ya shule kwa kuichoma moto.
Simbachawene alitoa amri hiyo jijini Mwanza, alipofanya ziara ya kikazi yenye lengo la kuimarisha utendaji kazi wa jeshi hilo pamoja na ushiriki wa wananchi katika kujua namna ya kujikinga na majanga ya moto.
Alisema mkoa huo una shida hususani katika masuala ya hujuma kwa kuwa matukio ya moto ni mengi hadi kufikia 93 jambo ambalo siyo sahihi ni lazima kuongezwe juhudi za kuhakikisha yanapungua.
"Matukio ya moto kwenye shule ni utundu wa vijana wanaanza kuhujumu miundombinu kwa sasa na wanafunzi watakaobainika kufanya uhalibifu wowote mkubwa wenye madhara katika shule wachukuliwe hatua," alisema Simbachawene
Aidha, Simbachawene aliwaagiza wakuu wote wa zimamoto nchini kuwaandikia barua ya kuwakumbusha wakurugenzi wa halmashauri na majiji ambao hawajanunua magari ya zima moto kuyanunua.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa Mkoa wa Mwanza,, Kamanda wa Jeshi la Zimamoto mkoani humo, Ambwene Mwakibete, alisema matukio ya moto na uokoaji kuanzia Julai 2020 hadi April 2021 yalifikia 93.
Aidha, alifafanua kwamba matukio ya moto ni 83 na ya uokoaji 10, vifo 13 na majeruhi 10 na wamefanya uchunguzi wa matukio 10.
Mwakibete alisema katika uchunguzi walibaini vyanzo vya matukio hayo ya moto ni umeme, hujuma na uzembe na kwamba kwa kushirikiana na vyoimbo vingine vya usalama wanaendelea kutoa elimu.
"Tunakabiliwa na changamoto ya visima vya maji ya kuzimia moto, maana mkoa una jumla ya visima 225 na kwamba 66 vinafanya kazi na 159 ni vibovu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.