Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John Magufuli ametoa salamu za pole kwa waandishi wa habari mkoani hapa hususani waliopata ajali katika Kijiji cha Kasuguti wilayani Bunda.
Ajili hiyo iliyotokea septemba 4 katika Ziara ya Mhe.Rais akielekea Wilayani Ukerewe kutekeleza ilani ya chama cha mpinduzi ya mwaka 2015.
Aidha, ajali hiyo ilihisisha gari aina ya STL 3530 na waandishi waliopata madhara ni Tunu Hermani (Uhuru FM), Rose Jacob (Tanzanite), Pius Rugonzibwa ( Dairy News), Neema Emmauel ( Nipashe), Katabazi Ismail ( Channel Ten) , Emmanuel Meshack (TVE) , Mashaka Balthazar ( Uhuru) na Abdul Salum ( Mahasin TV).
Akiwasilisha salamu hizo kwa niaba ya Mhe. Rais Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella alisema Mhe. Rais ameguswa na ajali hiyo kwani anatambua umuhimu wao katika kusukuma gurudumu la maendeleo nchini.
"Hakuna aliyetegemea ajali itatokea ila kutokana na hali ilivyo kwa sasa ya kiangazi ambapo vumbi lilipelekea madereva kushindwa kuona mbele hali iliyopelekea ajali mpaka sasa waandishi wote waliopata ajali wamepatiwa matibabu na kuruhusiwa na wanaendelea vyema pia natoa pole kwa wote waliokubwa na ajali hiyo," alisema Mongella.
Pia alitumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kumpokea Mhe. Rais wakati wa ziara mkoani hapa na kuwataka kuendelea kuunga mkono juhudi zake kwa kufanya kazi na kumuombea.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.