"Amani ni tunu muhimu ni lazima ilindwe kwa namna yoyote bila amani hakuna mafanikio."
Hayo Yamesemwa na Jumuiya ya Maridhiano Mkoa wa Mwanza katika tamko lao lililotolewa ukumbi wa Mwanza Hotel-kipepeo hii leo.
Akizungumza kwa niaba Jumuiya ya maridhiano Tanzania Mkoa wa Mwanza katibu Msaidizi Zuhura Mohamed alisema amani ni tunu muhimu ambayo inapaswa kulindwa kwa namna yeyote .
Alisema bila amani hakuna mafanikio ,pia aliwakumbusha watanzania kumchagua kiongozi atakaye thamini amani na kuilinda kwa maslahi ya nchi.
Naye Mratibu wa Jumuiya hiyo Askofu Richard Kamara alisema sote tunawajibika kutunza amani ambayo ina misingi mitatu ambayo ni haki ,upendo na utu ambavyo vinashikamana kujenga misingi ya nchi .
Alisema wagombea wote kwa nafasi yeyote waheshimu misingi ya nchi ili kuleta maendeleo pia watambue sio wagombea wote wanaweza kuwa viongozi jukumu la kila Mtanzania ni kumchagua kiongozi mwenye tija.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Alhaji Sheikh Mussa Kalwanyi alisema wanashirikiana na vyombo vya usalama na serikali kutatua migogoro ili kunusuru viashiria vya uvujifu vya amani,unyanyasaji katika Jamii .
" Kwa nafasi yetu kama wadau wa amani tuna haja ya kujitokeza pindi viashiria hovu vitakapoonekana ,tumepata fununu na kusikia kuna viashiria vya uvunjifu wa amani kama Mara,Mbeya tukiviacha hivi vikienea katika nchi yetu itakuwa siyo Jambo jema ndio maana tunaanza kulikemea" alieleza Sheikh Kalwanyi.
Naye Rehema Rajabu alisema viongozi wakubaliane na matokeo na wasisababishe vurugu kwani watakaoathiriwa ni wanawake,watoto,wazee hivyo Jambo la muhimu ni kufanya kampeni ya amani kama ilivyo nchi yetu huku wakitambua baada ya uchaguzi maisha yanaendelea.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.