Mwenge wa Uhuru leo Agosti 28, 2025 umezindua maduka 20 ya biashara pamoja na Jengo la duka kubwa la dawa muhimu katika soko la Ngudu Wilayani Kwimba vilivyojengwa kwa thamani ya zaidi ya Milioni 168 kama mradi wa kudumu wa ukusanyaji mapato ya ndani.
Akizindua Mradi huo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 Bw. Ismail Ali Ussi amewapongeza Viongozi wa Wilaya hiyo kwa kubuni chanzo cha kudumu cha kuongeza wigo wa ujusanyaji wa mapato kwa Halmashauri hiyo.
Amesema mradi huo una tija kubwa katika kuikuza Kwimba kwani kupitia tozo kama Kodi za kupangisha, Leseni za biashara, Kodi za huduma kama usafi na choo vitakua endelevu na kuisaidia Halmashauri hiyo kukusanya fedha ambazo zitasaidia kuboresha mazingira ya soko hilo lakini pia kutekeleza miradi mingine ya huduma za jamii.
Amesema mradi huo ni miongozi mwa miradi inayoenda kuwapa hadhi Ngudu na Halmashauri kwa ujumla na kuweza kupeleka hata kupandishwa hadhi kwa mji wa Ngudu.
Akitoa taarifa kwa niaba ya Mkurugenzi, Afisa Biashara wa Halmashauri hiyo Bi. Salome Mwaipopo amesema wameamua kujenga maduka hayo ili kuongeza vyanzo vya mapato na kwamba chanzo hicho pekee wamelenga kukusanya zaidi ya Tshs. Milioni 41 kwa mwaka.
Kadhalika, Kiongozi huyo ametoa wito kwa wananchi kujiandaa kushiriki katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 29 Oktoba, 2025 kwa amani na utulivu.
Awali, Mwenge wa Uhuru umekagua huduma za matumizi ya nishati safi ya kupikia pamoja na ujenzi wa bweni la wavulana katika shule ya Sekondari Ngudu vilivyogharimu zaidi ya Tshs. milioni 175 kabla ya kutembelea mashine ya kuongeza virutubishi kwenye nafaka pamoja na mradi wa vijana washonaji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.