Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella amepokea ugeni kutoka Korea ya Kusini (HOJUNG SOLUTION CO. LTD) uliofika Mkoani Mwanza,wilaya ya Ilemela kwa ajili ya majaribio na mafunzo ya upimaji wa ardhi kwa kutumia ndege ndogo(Drone) yenye uwezo wa kupima kilomita za mraba 6 kwa dakika 90 yatakayodumu kwa mwaka mmoja na kujumuisha wataalam wa ardhi Mkoa wa Mwanza.
Akipokea wataalam kutoka kampuni hiyo,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amesema ameridhishwa na kampuni mpango wa majaribio wa kampuni hiyo ambayo inatumia tekinolojia ya kidigitali kupima eneo kubwa kwa muda mfupi na kwa gharama nafuu na hii itapunguza usumbufu ambao umekuwa ukijitokeza wakati wa upimaji ikiwa ni pamoja na malalamiko ya wananchi.
“Nimeridhishwa na jaribio hili la mazoezi ya upimaji kwa kutumia ndege ambao utarahisisha ukusanyaji wa taarifa,picha,kuweka alama kwenye maeneo,ukusanyaji wa takwimu na kupunguza migogoro ya ardhi na kurahisisha upimaji na uandaaji wa ramani za Mipango Miji”.
Ilemela ina mahusiano mazuri na Korea ya Kusini.Uwepo wa mradi huo utasaidia ukusanyaji wa taarifa za ardhi,upimaji na upigaji wa picha ambapo baada ya majaribio hayo itapeleka taarifa serikalini ili kuelezea mafanikio na changamoto yaliyotokana na majaribio hayo kwa ajili ya maamuzi ikiwa itaridhia kufunga mkataba na Kampuni hiyo kwa ajili ya kufanya upimaji wa maeneo mengine.
Majaribio hayo yataanzia katika Manispaa ya Ilemela kwa maeneo ya Nyamadoke na Kahama na baadaye kuendelea wilaya ya Nyamagana lengo ikiwa ni upimaji wa eneo lote la Mkoa wa Mwanza.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.