LENGO LANGU KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU WA ELIMU NI KUINUA KIELIMU MKOA WA MWANZA-RC MAKALLA
*Nipo mbioni kuitisha kikao kikubwa na wadau wa Elimu ili kupanga mikakati ya Mwanza kuwa bora kielimu*
*Aipongeza Serikali kwa kuendelea kuiboresha Sekta ya Elimu nchini*
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.CPA.Amos Makalla amesema kwa kushirikiana na Wadau wa Sekta ya Elimu atahakikisha anauinua Mkoa huo kielimu ukiwa ni mkakati wa kuiunga mkono Serikali inayoendelea kuiboresha Sekta hiyo.
Akizungumza leo Ofisini kwake na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolph Mkenda, Mkuu huyo wa Mkoa amebainisha ili kuwa na Taifa imara lenye kujiamini kimaendeleo elimu ndiyo msingi wa yote hivyo hana budi kuwa na mikakati endelevu ya Mwanza kuwa kinara kielimu.
"Mhe.Waziri hivi karibuni nina mpango wa kukutana na wadau wa elimu Mkoani Mwanza ili tuzungumze kwa pamoja na kuweka mikakati madhubuti ya Mkoa huu kuwa bora kielimu," CPA Makalla.
Kwa upande wake Mhe. Prof Mkenda amesema ziara yake Mkoani Mwanza na Mara ni kujiridhisha na Maendeleo yanayofanywa na Wizara yake ikiwemo kukagua ujenzi wa Chuo cha Teknolojia Da re-s-Salaam Tawi la Mwanza.
"Pale Butimba leo Mhe. Mkuu wa Mkoa nitafungua Mafunzo Endelevu kwa Walimu Kazini (MEWAKA) yanayotolewa kwa Maafisa elimu kata kutoka Mikoa nane ya Tanzania Bara, yote hii ni mikakati ya Serikali kuhakikisha tunainua Sekta ya Elimu," amesisitiza Mhe. Prof Mkenda.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.