MAAFISA UGANI ONGEZENI BIDII VIJIJINI:DC NYANG'WALE
Maafisa Ugani wametakiwa kuongeza huduma zaidi vijijini kwenye idadi kubwa ya wakulima ambao baadhi yao bado hawana kilimo chenye tija.
Rai hiyo imetolewa leo Agosti 7,2024 na Mkuu wa Wilaya ya nyang'wale kutoka mkoani Geita,Mhe.Grace Kingalame alipofanya ziara fupi ya kutembelea mabanda ya Nanenane eneo la Nyamhongolo mkoani Mwanza na kubainisha kutokana na kutopata elimu ya kitaalamu baadhi ya wakulima wanatumia nguvu nyingi na kupata mazao hafifu.
"Maonesho haya nimefurahishwa kuwepo na elimu kwa wakulima kutokana na Taasisi nyingi zinazojihusisha na kilimo mabanda yao kuwepo na wataalamu,sasa wasiishie mijini tu bali waje vijijini",Kingalame
Amesema Mhe.Rais Samia ameonesha dhahiri mkakati wake wa kuinua sekta ya kilimo kwa kuweka fedha nyingi ili wananchi wafaidike na kilimo cha kisasa na chenye tija.
Amewapongeza pia waandaaji wa maonesho hayo mikoa ya Kanda ya Ziwa Magharibi Mwanza,Kagera na Geita kutokana na mwamko mzuri wa wananchi unao wawezesha pia kujiongezea kipato.
Maonesho hayo yatafikia kilele Agosti 8 mwaka huu mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Said Mtanda.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.